Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Pwani (kwa Kifaransa: Littoral) ni moja ya mikoa kumi na mbili ya Benin. Ndio mkoa mdogo zaidi kati ya mikoa yote nchini. Una manispaa moja tu ambayo ni mji mkuu Cotonou, jiji kubwa zaidi nchini na kitovu cha uchumi wake.
Littoral ilitengwa mkoa wa Atlantique mnamo 1999.