Mkoa wa Kati, Togo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Kati (Centrale)
Wilaya za Mkoa wa Kati

Mkoa wa Kati (Kifar. Region Centrale) ni mojawapo ya mikoa mitano nchini Togo katika Afrika Magharibi. Makao makuu yapo mjini Sokode.

Mkoa wa Kati ndio eneo lenye watu wachache zaidi nchini Togo lenye jumla ya watu 617,871 kulingana na sensa iliyofanyika mwaka wa 2010. [1]

Miji mingine katika eneo la Mkoa wa Kati ni pamoja na Tchamba na Sotouboua .

Mkoa wa Kate umegawanywa katika wilaya za Blitta, [2] Sotouboua, Tchamba, Tchaoudjo na wilaya ndogo (subprefecture) Mö.

Mkoa wa Kati uko kaskazini mwa Mkoa wa Plateaux na kusini mwa Mkoa wa Kara. Kama maeneo mengine ya Togo, inapakana na Ghana upande wa magharibi na Benin upande wa mashariki.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Law, Gwillim. "Regions of Togo". Statoids.com. Gwillim Law. Iliwekwa mnamo 11 April 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Annuaire Statistique du Togo (2010-2013)" (kwa Kifaransa). October 2019. Iliwekwa mnamo 2021-08-06.  Check date values in: |date= (help)