Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Kara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Kara nchini Togo
Wilaya za Kara

Mkoa wa Kara ni mojawapo ya mikoa mitano ya Togo. makao makuu ya mkoa yako mjini Kara.

Mkoa una eneo la kilomita za mraba 11,738. Idadi ya wakazi imekadiriwa kufikia 957,600 kwenye mwaka 2020.[1]

Miji mingine katika eneo la Kara ni pamoja na Bafilo, Bassar, na Niamtougou .

Mkoa wa Kara umegawanywa katika wilaya za Assoli, Bassar, Bimah, Dankpen, Doufelgou, Keran, na Kozah .

Kara iko kaskazini mwa Mkoa wa Kati na kusini mwa Mkoa wa Savanes. Upande wa magharibi iko Ghana, na upande wa mashariki iko Benin .

  1. https://www.citypopulation.de/en/togo/cities/ Togo-Regions, tovuti ya citypopulation.de