Mkoa wa Plateaux, Togo
Mkoa wa Plateaux ni mojawapo ya mikoa mitano ya Togo . Plateaux iko kaskazini mwa Mkoa wa Maritime na kusini mwa Mkoa wa Kati (Centrale). Jina "Plateaux"[1] linamaanisha nyanda za juu. Mlima Agou (mita 986) ni sehemu ya juu nchini Togo.
Mkoa huo una eneo la kilomita za mraba 16,975. Idadi ya wakazi kwenye mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa 1,705,300.[2]
Makao makuu ya mkoa yako mjini Atakpame. Plateaux ni mkoa mkubwa zaidi kieneo na ina idadi ya pili ya wakazi baada ya Mkoa wa Maritime.
Miji mingine mikubwa katika eneo la Plateaux ni pamoja na Kpalime na Badou.
Upande wa magharibi mkoa unapakana na Ghana na upande wa mashariki unapakana na Benin.
Plateaux imegawanywa katika wilaya za Agou, Amou, Danyi, Est-Mono, Haho, Kloto, Moyen-Mono, Ogou na Wawa.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ tamka "platoo"
- ↑ https://www.citypopulation.de/en/togo/cities/ Togo, Regions; tovuti ya citypopulation.de