Mzingo elektroni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mizingo elektroni)
Mfano wa atomu ya natiri Na (sodiamu) yenye mizingo mitatu

Mzingo elektroni (kwa Kiingereza: electron shell) ni maeneo ya atomi ambayo kikemia elektroni hukadiriwa kupatikana humo, maeneo haya huchukua maumbo ya duara yakikizunguka kiini cha atomi ndani ya elementi.

Duara hizi hudhaniwa kuwa kama obiti. Kila obiti au mzingo huwa na idadi ya juu ya elektroni zinazoweza kuzunguka mle: mzingo wa kwanza (wa ndani zaidi, iliyo karibu zaidi na kiini) hupokea elektroni hadi 2, mzingo wa pili hadi 8, mzingo wa tatu hadi 18.

Elektroni kwenye mzingo wa nje zinatawala tabia za kikemia za atomu. Mzingo huo ni mzingo valensi unaotawala valensi yaani uwezo wa atomu kushikana na atomu nyingine.

Kama mzingo wa nje unajaa nafasi zote ni atomu thabiti ambazo hazimenyuki kirahisi na elementi nyingine, kwa mfano gesi adimu au metali adimu.


Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzingo elektroni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.