Mitumba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mitumba ni neno la Kiswahili, ambalo maana yake halisi ni "vifurushi", na linalotumiwa kurejelea vifurushi vilivyofungwa vya plastiki vya nguo zilizotolewa na watu katika nchi tajiri. Neno hili pia linatumika katika mavazi ambayo hufika kwenye vifurushi hivyo.

Moja ya bandari kuu inayopokea mitumba ipo nchini Tanzania jiji la Dar es Salaam. Kutoka hapo mavazi yanatawanywa ndani ya bara la Afrika.

Usafirishaji na uuzaji wa mitumba unafanyika kwa namna nyingi katika kampuni tajiri na katika nchi za Afrika ambapo mitumba inanunuliwa na kuuzwa.

Wakosoaji wa biashara ya mitumba wanaona kuwa uwepo wa nguo za bei nafuu unachangia kudorora kwa viwanda vya nguo vya ndani. [1]

Wafuasi wa mitumba wanaeleza kuwa mavazi hayo yana manufaa kwa kuwa yanachochea shughuli za kiuchumi na kuwaruhusu watu wenye uwezo mdogo kumudu mavazi ya mtindo. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "East Africa's used-clothes trade comes under fire". 
  2. Germany, SPIEGEL ONLINE, Hamburg. "GLOBALISIERUNG: Das Hemd des toten Weißen - DER SPIEGEL 2/2006". www.spiegel.de (kwa Kijerumani). Iliwekwa mnamo 2017-07-30. 
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mitumba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.