Mishamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mishamu jinsi inavyotokea katika ardhi
Kiko cha mishamu, jinsi kilivyochongwa Uturuki

Mishamu (pia sepioliti, meerschaum) [1] ni madini laini meupe, ambayo hutumiwa kutengeneza viko vya tumbaku (maarufu kama kiko cha mishamu). Mishamu ni silikati ya magnesi yenye fomula Mg4Si6O15(OH)2 · 6H2O, inaweza kupatikana kwa umbo la nyuzi, chembechembe, na hali ngumu.

Iligunduliwa na kupewa jina la meerschaum na Abraham Gottlob Werner mnamo 1788. Neneo hilo la Kijerumani linamaanisha povu la bahari, maana inaweza kuwa nyepesi hadi kuelea juu ya maji. Mnamo 1847 Mjerumani mwingine alipendekeza jina la sepioliti alipoikuta pale Italia, kufuatana na mifupa na ngisi.

Upatikanaji[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya akiba za kibiashara inapatikana hasa kutoka tambarare ya Eskişehir nchini Uturuki, kati ya Istanbul na Ankara . Inachimbwa hapa katika migodi midogo.

Katika Afrika ya Mashariki, mishami hupatikana Tanzania tangu siku za ukoloni katika maeneo ya Ziwa Amboseli .

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]