Nenda kwa yaliyomo

Kiko (kifaa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Viko tofautitofauti.

Kiko (pia: toza au mtemba) ni chombo kinachomwezesha mtu kuvuta moshi wa tumbaku, bangi au bidhaa nyingine za uraibu zinazovutwa kama sigara. Kiko huwa na digali au mrija uliounganika na kijibakuli.

Sehemu tofauti za kiko[hariri | hariri chanzo]

Sehemu tofauti za kiko: (1) kibakuli, (2) chemba, (3) shimo la kupitisha moshi, (4) shina linaloshikana na kibakuli, (5) tunduunganishi la kiko, (6) ulimi unaoingia kwenye tunduunganishi, (7) shina la ncha ya kufyonzia, (8) mdakale wa kufyonzia, (9) mdomo wa mrija, na (10) shimo inayopitisha moshi.

Kiko huwa na sehemu tofautitofauti za kuwezesha mtumiaji kuvuta tumbaku na pia kuisafisha. Viko vingi huwatoanishwa ncha ya kibakuli na ncha ya kuvyozia ili kuwezesha usafishaji kwa urahisi. Ncha ya kibakuli ndiyo sehemu yenye kibakuli kinachowekwa chembechembe za tumbaku au bangi na kuashwa. Ncha ya kufyonzia ndiyo huwekwa mdomoni.

Utendakazi wa kiko[hariri | hariri chanzo]

Tumbaku au bangi huwekwa na kuchomwa kwenye kibakuli, naye mraibu anaivuta moshi kupitia mdomo ulio kwenye ncha ya mrija.

Aina ya viko[hariri | hariri chanzo]

Aina ya viko kulingana na asili[hariri | hariri chanzo]

 • Kiseru - kiko cha Japani
 • Sebsi - kiko cha tumbaku cha kitamanduni cha Moroko
 • Midwakh - kiko cha Kiarabu
 • Chibouk - kiko chenye mrija mrefu cha Uturuki

Aina ya viko kulingana na muundo[hariri | hariri chanzo]

 • Paipu ya kuvutia tumbaku (maarufu kama Chillum) - tofauti kidogo na viko vingine kiko hiki hakina kibakuli bali kina mrija na chembechembe za tumbaku huekwa upande mmoja wa mrija unaowashwa naye mtumiaji anavuta moshi upande ule mwingine.
 • Buruma (hujulikana kama Hookahs) - kiko kikubwa chenye jipipa la maji na shilamu au mdakale mrefu. Hutumika sana sana kwenye uvutaji wa shisha

Aina ya viko kulingana na nyenzo[hariri | hariri chanzo]

 • kiko cha chuma -kiko kilichoundwa na chuma sana sana alumini
 • kiko cha gilasi
 • kiko cha mboko
 • kiko cha kauri[1][2]
 • kiko cha mishamu
 • kiko cha gunzi la mahindi[3]

Aina ya viko kulingana na matumizi[hariri | hariri chanzo]

 • Kibong'i - kiko cha kuvutia bangi au tumbaku chenye uwezo wa kuchunja moshi kwa kuupitishia kwa maji
 • Kiko cha afyuni - kiko maalum cha kuvukisha na kuvuta mivuke ya afyuni
 • Kiko cha kiputo - kiko cha watoto cha kuchezea kinacho puliza tone la hewa katika kioevu

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Cambridge Archaeology Field Group. "Evolution of clay tobacco pipes in England" (PDF). Cambridge Archaeology Field Group (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-10-07.
 2. Newns, S. The Clay Tobacco Pipes in N. Corcos et al. Excavations in 2014 at Wade Street, Bristol - a documentary and archaeological analysis, Internet Archaeology 45. https://doi.org/10.11141/ia.45.3.4 Iliwekwa mnamo 2018-20-07
 3. "History of Missouri Meerschaum Company - The world's oldest and largest manufacturer of corn cob pipes. - Washington, MO". corncobpipe.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2001-05-09. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help) Iliwekwa mnamo 2018-10-07.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiko (kifaa) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.