Mpopi
Mpopi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Mpopi (kutoka Kiing. "poppy"; jina la kitaalamu: Papaver somniferum) ni mmea wenye asili katika nchi za Mashariki ya Kati. Inakua hadi urefu wa mita 1 ikiwa na maua meupe, manjano na mara nyingi mekundu. Mpopi ni asili ya madawa ya kulevya ya afyuni na heroini yanayotumiwa pia kama madawa ya tiba hasa kwa kutuliza maumivu makali.
Mbegu zake hutumiwa kwa kutoa mafuta pia kama chakula ukichanganywa ndani ya keki na mikate.
Kemikali zinazosababisha matumizi ya afyuni ziko hasa katika utomvi wa mpopi lakini kwa kiasi kidogo pia kwenye majani na mbegu wake. Afyuni hutengenezwa kwa kukata tumba za ua la mpopi; utomvi mweupe unatoka nje na kuganda hewani kuwa masi kama mpira. Masi hii ni afyuni bichi.
Afyuni hulimwa hasa kwa ajili ya biashara haramu ya afyuni na heroini. Nchi yenye mashamba makubwa ni Afghanistan na Myanmar. Hata kama kilimo na biashara hii ni haramu wakulima maskini wanavutwa na mapato ambayo ni juu kuliko mapato kutokana na mazao ya chakula.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- The Heroin Harvest Ilihifadhiwa 11 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.
- Comprehensive profile for Papaver somniferum Ilihifadhiwa 16 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine. from MaltaWildPlants.com
- Opium FAQ v1.0 Ilihifadhiwa 6 Oktoba 2012 kwenye Wayback Machine. from Opioids.com
- Opium Poppy Cultivation and Heroin Processing in Southeast Asia Ilihifadhiwa 26 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine. from the School of Pacific and Asian Studies
- "Downward Spiral - Banning Opium in Afghanistan and Burma", Transnational Institute TNI, Debate Paper, June 2005