Minou
Mandhari
"Minou" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Orchestra Marquis Original | ||
Umetolewa | 1992 | |
Umerekodiwa | 1992 | |
Aina ya wimbo | Muziki wa dansi | |
Lugha | Kiswahili | |
Urefu | 8:13 | |
Mtunzi | Tshimanga Assossa | |
Mtayarishaji | Tshimanga Assossa |
Minou ni jina la kutaja wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Marquis Original kati ya miaka ya tisini. Wimbo ulitolewa mwaka wa 1992. Mashairi yake anamsihi mke wake wasiachana na kuwambia abadili uamuzi wake kwa amemzoea sana. Pamoja na kulazimisha talaka, bado bibie aliendelea kumtangazia mbovu mitaani. Anamuonea huruma kwa wale waliomdanganya wamemkimbia na wamemwacha mtu hana hata pa kushikia.
Uchambuzi
[hariri | hariri chanzo]Mashairi
[hariri | hariri chanzo]Wewe ndiyo uliyoanza.. kunitaka eti tuachane.. Nilikubembeleza usiku kucha.. Ubadilishe uamuzi wako mama.. Nimekuzoea eeeh.. Hukutaka kunisikia.. Ukanihukumu bila hatia.. Ukanitangazia ubaya ulivyotaka.. We Minou eeh.. We Minou eeh..
Ona sasa wivu wako... Mwenzako mie masikini.. Nilijua eeeh.. Waliokudanganya wapo wapi.... Wamekuacha huna pa kuanzia.... Dunia ya leo matata... We Minou eeh.. We Minou eeh..
Wahusika
[hariri | hariri chanzo]- Mtunzi: Tshamanga Kalala Asossa
- Waimbaji: Tshimanga Asossa, Bobo Sukari, Freditto Butamu (marehemu) Mutombo Lufungula 'Audax' (marehemu) Mukumbule Lolembo 'Parash'.
- Mpiga solo: Kivukutu Moto na Tchacho.
- Besi: Ilunga Banza ' Mchafu'. (marehemu)
- Mpiga rhythim: Mulenga Kalonji 'Vata' (marehemu)
- Saxa: Berry Kankonde (marehemu)
- Tarumbeta: Kaumba Kalemba (marehemu)
- Ngoy Mubenga.
- Keyboard: Mbuya Makonga 'Adios'.
- Ngoma: Mharami Seseme