Hali Ngumu
Mandhari
"Hali Ngumu" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Marquis Original | ||
Umetolewa | 1989-1990 | |
Umerekodiwa | 1989-1990 | |
Aina ya wimbo | Muziki wa dansi | |
Lugha | Kiswahili | |
Urefu | 7:38 |
Hali Ngumu ni jina la wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Marquis Original katika miaka ya 1980 mwishoni na 1990 mwanzoni. Ni kati ya nyimbo zilizotamba sana katika miaka hiyo.
Mashairi yake anazungumzia mkewe ambaye analalamikia maisha magumu na kutoa siri za ndani, yaani, mambo ya mume na mkewe. Hivyo basi anamsihi wakumbuke walipotoka na asiwasikilize hao vijino pembe.
Hivyo basi abadili mwenendo wake na atakachopata atamtimizia, zaidi ya hapo hawezi kwani maisha yake yatakwenda kombo.
Wahusika
[hariri | hariri chanzo]- Mpiga Solo - Dekula Kahanga
- Mpiga Solo la 2 - Steven Kaingilila
- Mpiga rythm - Mulenga Kalonji
- Mpiga besi - Banza Mchafu
- Mpiga Dramz - Mharami Seseme
- Mpiga Congas - Seif Said
- Mpiga Sax - Berry Kankonde na Mukuna Roy
- Mpiga Tarumbeta - Kaumba Kalemba
- Mtunzi wa wimbo - Ngoie Mubenga
- Waimbaji: Issa Nundu, Parash Mukumbule, Mutombo Audax na Tshimanga Assosa.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Hali Ngumu katika YouTube