Michelle Rodriguez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michelle Rodriguez
Rodriguez mnamo 2013
Rodriguez mnamo 2013
Jina la kuzaliwa Mayte Michelle Rodríguez
Alizaliwa 12 Julai 1978
Marekani
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1999 - hadi leo
Wazazi Carmen Milady,
Rafael Rodriguez
Tovuti Rasmi michelle-rodriguez.com

Mayte Michelle Rodriguez[1] alizaliwa 12 Julai 1978[2] anayejulikana kuigiza filamu kama Girlfight, The Fast and The Furious, Blue Crush, Resident Evil, S.W.A.T., na Avatar. Vilevile, ameigiza kama Ana Luzia Cortez kwenye kipindi cha Lost.

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Rodriguez alizaliwa mjini Bexar County, Texas. Yeye ni mtoto wa Carmen Milady na Rafael Rodriguez - aliyefanya kazi kwa jeshi la Marekani.[3] Rodriguez alihamia nchini Dominican Republic alipokuwa na miaka minane pamoja na mamake na akaishi Puerto Rico mpaka alipofika miaka kumi na moja, na baadaye kuhamia mjini New Jersey. Rodriguez alijiunga na chuo kikuu na kusomea biashara lakini akaiacha na kujiunga na shule ya uigizaji, akiwa na azma ya kuwa mwandishi wa filamu.[4]

Uigizaji[hariri | hariri chanzo]

Rodriguez kwenye sherehe ya New York Fashion Week mnamo 2006
Filamu
Mwaka Filamu Aliigiza kama Maelezo
2000 Girlfight Diana Guzman
2001 The Fast and the Furious Letty
3 A.M. Salgado
2002 Blue Crush Eden
Resident Evil Rain Ocampo
2003 S.W.A.T. Chris Sanchez
2004 Control Teresa
2005 BloodRayne Katarin
2006 The Breed Nicki
2007 Battle in Seattle Lou
2008 A Cat's Tale Jujube Sauti
Gardens of the Night Lucy
2009 Fast & Furious Letty
Trópico de Sangre Minerva Mirabal
Avatar Trudy Chacon
2010 Machete Luz
2011 Battle: Los Angeles Corporal Adriana Santos
Army of Two Alice Murray
2012 Resident Evil: Retribution Rain Ocampo
Filamu
Mwaka Jina Aliigiza kama Vipindi
2005 Punk'd Mwenyewe 1
Immortal Grand Prix Liz Ricarro 26
2005-2006, 2009 Lost Ana Lucia Cortez 25
2007 Adventures in Voice Acting Mwenyewe 1

Mashtaka[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Machi 2002, Rodriguez alifungwa kwa ajili wa kumpiga rafiki yake.[5] Madai haya yalitolewa pindi aliyempiga alipokataa kwenda kutoa ushahidi mahakamani.[6] Mnamo Juni 2004, Rodriguez alishtakiwa kwa kuendesha gari ilhali alikuwa amelewa.[7] Alipelekwa rumande kwa masaa 48.

Mnamo 2005, alipokuwa anarekodi Lost mjini Hawaii, alishikwa mara kadhaa na polisi kwa ajili ya kuvunja sheria barabarani na akatozwa faini ya $357.[8]

Maisha ya kibinafsi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 2000, alipendana na Muislamu lakini akaachana naye akisema kuwa dini hiyo ina sheria nyingi.[9] Mnamo 2003, Rodriguez ameonekana akiwa na muigizaji Olivier Martinez nchini Ufaransa.[10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Official Site Biography. Michelle-Rodriguez.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-05-16. Iliwekwa mnamo 2007-02-07.
  2. Rebecca Flint Marx (2008). Michelle Rodriguez:Biography. MSN. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-07-28. Iliwekwa mnamo 2008-08-27.
  3. Michelle Rodriguez Biography (1978-). Film Reference. Iliwekwa mnamo 2007-12-25.
  4. Michelle Rodriguez Official Biography. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-05-16. Iliwekwa mnamo 2008-06-06.
  5. Grossberg, Josh. ""Girlfight" Star Busted for Girl Fight", E!, Comcast, 2002-03-20. Retrieved on 2007-02-04. 
  6. Grossberg, Josh. ""Girlfight" Star Off the Hook", E!, 2002-04-08. Retrieved on 2007-02-04. 
  7. "'Lost' Actress Chooses Jail Over Service", Associated Press, 2006-04-26. Retrieved on 2006-07-21. Archived from the original on 2007-10-13. 
  8. "Michelle Rodriguez settles two traffic cases", Associated Press, 2005-12-14. Retrieved on 2006-07-21. 
  9. Rodriguez Turned Down Muslim Marriage (2008-06-06).
  10. Minogue's Martinez linked to Rodriguez. Contact Music (2008-05-02). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-02-18. Iliwekwa mnamo 2005-03-03.