Mfalme Manase

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mfalme Manase alikuwa mfalme wa Ufalme wa Yuda.

Alikuwa mwana pekee wa Hezekia na mkewe Hefzibah.

Alipata kuwa mfalme akiwa na umri wa miaka 12 akatawala kwa miaka 55 (2 Wafalme 21:1; 2 Mambo ya Nyakati 33:1).

Edwin Thiele amesema kuwa Manase alianza kutawala pamoja na baba yake, Hezekia mwaka 697/696 KK, na utawala wake pekee ulianza 687/686 KK na kuendelea mpaka kufa kwake 643/642 KK.

William F. Albright amesema kwamba utawala wa Manase ulikuwa miaka 687-642 KK.

Historia ya Biblia kuhusu Manase inapatikana katika 2 Wafalme 21:1-18 na 2 Mambo ya Nyakati 32:33-33:20. Pia ametajwa katika Yeremia 15:4.

Mfalme Manase alimuoa Meshullemeth, nao walikuwa na mwana aliyeitwa Amoni.

Hezekia, Manase na Amoni wametajwa katika vizazi vya ukoo wa Yesu katika Injili ya Mathayo, 1:1-17.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfalme Manase kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.