Nenda kwa yaliyomo

Meli kubwa duniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Meli kubwa duniani siku hizi ni meli za mizigo hasa zinazobeba mafuta ya petroli au kontena, lakini pia meli za abiria zinazobeba watalii kwa burudani. Kuna pia meli chache zenye kusudi maalumu kama MS Pioneering Spirit ambayo ni meli kubwa ya winchi kwa ujenzi baharini.

Seawise Giant ilikuwa meli kubwa iliyotengenezwa hadi leo (2018); hapa wakati wa ukarabati 1990 huko Singapur

Meli kubwa kabisa iliyojengwa hadi sasa ilikuwa Seawise Giant yenye tani GT 564,763 na urefu wa mita 458. Ilitengenezwa mwaka 1974-1979 nchini Japani kwa kampuni ya Kigiriki na kurefushwa baadaye hadi kufikia mita 458. Kutokana na ukubwa wake haukuweza kupita wala katika Mfereji wa Suez wala katika Mfereji wa Kiingereza. Miaka yake ya mwisho ilitumiwa kama tangi ya mafuta tu bila kusafiri tena. Mwaka 2009 ilivunjika.

Orodha ya meli kubwa duniani mnamo mwaka 2018

[hariri | hariri chanzo]
Jina inabeba Urefu Kina chini ya uso wa maji Tani GT Wajenzi Wamiliki ref
Pioneering Spirit winchi na karahana mita 382 mita 10–15 403,342 Daewoo Shipbuilding & Marine Engineering Allseas [1]
FSO Asia mafuta mita 379 mita 24.525 234,006 Daewoo Shipbuilding & Marine Engineering Tankers International
FSO Africa mafuta mita 379 mita 24.525 234,006 Daewoo Shipbuilding & Marine Engineering Tankers International
TI Europe mafuta mita 379 mita 24.525 234,006 Daewoo Shipbuilding & Marine Engineering Tankers International
Seaways Laura Lynn mafuta mita 379 mita 24.525 234,006 Daewoo Shipbuilding & Marine Engineering Tankers International
Symphony of the Seas abiria mita 361.011 mita 9.322 228,081 STX France SA Royal Caribbean International [2]
Harmony of the Seas abiria mita 362.1 mita 9 226,963 STX France SA Royal Caribbean International [3]
Oasis of the Seas abiria mita 360 mita 9 225,282 STX Turku Shipyard Royal Caribbean International [4]
Allure of the Seas abiria mita 360 mita 9 225,282 STX Turku Shipyard Royal Caribbean International [5]
CMA CGM Antoine de Saint Exupery kontena mita 400 mita 16 217,673 Hanjin Heavy Industries and Construction Philippines CMA CGM [6]
CMA CGM Jean Mermoz kontena mita 400 mita 16 217,673 Hanjin Heavy Industries and Construction Philippines CMA CGM
Ever Golden kontena mita 400 mita 16 217,612 Imabari Shipbuilding Saijo Evergreen Marine [7]
Ever Genius kontena mita 400 mita 16 217,612 Imabari Shipbuilding Saijo Evergreen Marine
Ever Goods kontena mita 400 mita 16 217,612 Imabari Shipbuilding Marugame Evergreen Marine [8]
Madrid Maersk kontena mita 399 mita 16 214,286 Daewoo Shipbuilding and Marine Engineering Maersk [9]
Munich Maersk kontena mita 399 mita 16 214,286 Daewoo Shipbuilding and Marine Engineering Maersk [10]
  1. Pioneering Spirit kwenye tovuti ya allseas.com
  2. "Symphony of the Seas (34719)". DNV GL Vessel Register. Det Norske Veritas. Iliwekwa mnamo 2018-03-23.
  3. "Harmony of the Seas (33249)". DNV GL Vessel Register. Det Norske Veritas. Iliwekwa mnamo 2018-01-12.
  4. "Oasis of the Seas (27091)". DNV GL Vessel Register. Det Norske Veritas. Iliwekwa mnamo 2018-01-12.
  5. "Allure of the Seas (28329)". DNV GL Vessel Register. Det Norske Veritas. Iliwekwa mnamo 2018-01-12.
  6. "CMA CGM Antoine de Saint Exupery (9776418)". Veristar Info. Bureau Veritas. Iliwekwa mnamo 2018-02-23.
  7. "Ever Golden (18265349)". ABS Record. American Bureau of Shipping. Iliwekwa mnamo 2018-04-01.
  8. "Ever Goods (18265350)". ABS Record. American Bureau of Shipping. Iliwekwa mnamo 2018-06-06.
  9. "Madrid Maersk (17265397)". ABS Record. American Bureau of Shipping. Iliwekwa mnamo 2018-02-04.
  10. "Munich Maersk (17265398)". ABS Record. American Bureau of Shipping. Iliwekwa mnamo 2018-02-04.