McVitie's

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

McVitie's ni jina la kibiashara ya chakula inayomilikiwa na United Biscuits. Jina hili linapata asili kutoka muundaji wa biskuti wa Scotland, McVitie & Price Ltd, iliyoanzishwa katika mwaka wa 1830 Rose Street mjini Edinburgh, Scotland. Kampuni hii ilihamia maeneo mbalimbali ya jiji kabla ya kukamilisha,katika mwaka wa 1888,kiwanda cha kuunda biskuti cha St Andrews katika Robertson Avenue katika Wilaya ya Gorgie.

Nembo mpya ya McVitie's tangu 2005

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ingawa kiwanda cha McVitie & Price kilichomeka katika mwaka wa 1894,kilijengwa upya mwaka uo huo na kikaendelea kufanya kazi hadi 1969,wakati kazi ilisimaishwa humo na kuhamishwa Uingereza. McVitie & Price waliendelea na upanuzi na kuunda kiwanda kipya katika Harlesden(1910) na mjini Manchester (1917). Kampuni ilinunua jumba la uokaji la Edinburgh la Simon Henderson & Wana wake katika mwaka wa 1922. McVitie & Price ilijiunga na jumba jingine la uokaji la Scotland ,MacFarlane,Lang & Co.,mwaka wa 1948 ili kuwa Kundi la United Biscuits.

Bidhaa za McVitie's zinaundwa katika viwanda vitano vya Uingereza: viwanda viwili vya kitambo McVitie's vya Harlesden na Manchester, kiwanda cha kitambo cha MacFarlane,Lang & Co,kiwanda cha kuunda biskuti cha Victoria huko Glasgow,kiwanda cha kitambo cha Carr cha kutayarisha biskuti cha 1831Carlisle na kiwanda cha keki cha McVitie's(kiliitwa cha Riley's Toffee Works} huko Halifax.

Biskuti maarufu ya kwanza ya McVitie & Price ilikuwa McVitie's Digestive,biskuti ya aina hiyo ya kwanza kabisa,iliyoundwa na mfanyikazi mpya Alexander Grant. Biskuti hii ilipewa jina hilo kwa sababu kulifikiriwa kuwa soda ya kuoka ilikuwa inasaidia katika mfumo wa mwili wa kusaga chakula tumboni.

McVitie's Chocolate Homewheat Digestive iliundwa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1925. Zaidi ya pakiti milioni 71 ya McVitie's Chocolate Homewheat Digestive hununuliwa Uingereza kila mwaka,yaani biskuti 52 kulwa kila sekunde. HobNobs iliundwa katika mwaka wa 1985 na aina nyingine kama hiyo ya chokleti ikaundwa mwaka wa 1987.

Katika mwaka wa 1947,McVitie & Price ilioka keki ya harusi ya Malkia Elizabeth na Luteni Philip Mountbatten.

Baadhi ya bidhaa lya McVitie's ziliitwa McV mnamo mwaka wa 2002, lakini hii ilibadilishwa 2005 na toleo jipya la nembo ya McVitie's. Hapo mwaka wa 2007, United Biscuits iliipa leseni ya McVitie's kwa Meiji Seika Kaisha Ltd ili waweze kupika biskuti hizo Ujapani.


Bidhaa zao[hariri | hariri chanzo]

Biskuti[hariri | hariri chanzo]

Keki[hariri | hariri chanzo]

  • Keki ya Golden Syrup
  • Keki ya Jaffa
  • Keki ya Tangawizi ya Jamaica
  • Keki ya Lemon


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

1.^ a b The National Archives of Scotland , McVitie & Price, Ltd,, 2007-11-02

2. ^ United Biscuits , Historia yetu,2007-11-06

3.^ "Maeneo". United Biscuits. . 2007-08-16.

4. ^ "McVitie's". United Biscuits.. 2007-08-16.

5. ^ "Harusi ya Malkia".Habari ya BBC. 2008-01-15.

6. ^ "McVities Digestives ya Ujapani". nicecupofteaandasitdown.com. Retrieved 2007-08-16.


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]