Mbombela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mbombela
Mbombela is located in Afrika Kusini
Mbombela
Mbombela

Mahali pa mji wa Mbombela katika Afrika Kusini

Majiranukta: 25°28′12″S 30°58′48″E / 25.47000°S 30.98000°E / -25.47000; 30.98000
Nchi Afrika Kusini
Majimbo Mpumalanga
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 695,913
Mji wa Mbombela.

Mbombela (awali: Nelspruit) ni mji mkuu wa jimbo la Mpumalanga katika Afrika Kusini. Uko kando ya mto Crocodile (mamba) takriban km 330 upande wa mashariki wa Johannesburg na km 60 upande wa magharibi wa mpaka wa Msumbiji.

Mji wenyewe una wakazi 695,913 pamoja na vitongoji vilivyojenga wakati wa siasa ya apartheid viko mbali kidogo ni KaNyamazane, Msogwaba, Mpakeni na Matsulu.

Mbombela ni kitovu cha huduma na biashara kwa mazingira yenye kilimo kingi; kuna pia viwanda vinavyoshughulikia mazao kama machungwa, malimau, maembe, jozi na ndizi.

Kuna kituo cha reli pamoja na uwanja wa ndege. Kuna utalii kutokana na wageni wa hifadhi ya taifa ya Kruger iliyo karibu.

Mbombela ilikuwa mahali mojawapo pa kombe la dunia la soka mwaka 2010.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mbombela kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.