Maunzingumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bongo kuu inayoitwa PDP-11-M7270.

Maunzingumu (pia maunzi ngumu[1]; kwa Kiingereza: hardware) ni sehemu za kompyuta zinazoshikika . Maunzingumu ni vifaa mbalimbali vinavyounda mashine ya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu:

  1. vifaa vya kuingizia data (Input devices),
  2. vifaa vya kutolea data (Output devices) na
  3. vifaa katika tarakilishi (Kadi ya mtandao, Kadi ya sauti, diski kuu).

Maunzingumu haina kazi bila programu na data za maunzilaini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maunzingumu ni pendekezo la Kiputiputi katika kamusi ya KSK; orodha za Microsoft na Kilinux za 2004/05 zilitumia "maunzi" pekee, ling. [https://web.archive.org/web/20120806015358/http://www.kilinux.udsm.ac.tz/kiblog/documents/glossary/sw_TZ_Extended_glossary.xls Kilinux Extended Glossary], tovuti ya Kilinux kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2009), kupitia archive.org
  • Kiputuputi, Omari (2011). Kamusi Sanifu ya Kompyuta, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Toleo la Kwanza 2011, ISBN 978 9987 531 127