Maude Barlow
Maude Victoria Barlow (alizaliwa Mei 24, 1947) ni mwandishi na mwanaharakati wa Kanada. Yeye ni mwanachama mwanzilishi wa Baraza la Wakanada la utetezi wa wananchi lenye wanachama kote Kanada. [1] Yeye pia ni mwanzilishi mwenza wa Mradi wa Blue Planet, ambao unafanya kazi kimataifa kwa ajili ya haki ya maji kwa binadamu. Barlow ni mwenyekiti wa bodi ya shirika la Chakula na Maji lenye makao makuu mjini Washington, ni mwanachama mwanzilishi wa Jukwaa la Kimataifa la Utandawazi lenye makao yake mjini San Francisco, pia alikuwa Diwani katika Baraza la Dunia lenye makao yake mjini Hamburg. mnamo mwaka 2008 hadi 2009, aliwahi kuwa Mshauri Mkuu wa Maji kwa Rais wa 63 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na alikuwa kiongozi katika kampeni ya kutaka maji yatambuliwe kama haki ya binadamu na Umoja wa Mataifa. [2] [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Maude Barlow | The Council of Canadians". canadians.org. Iliwekwa mnamo 2017-01-09.
- ↑ Barlow, Maude. "Notes for UN Panel, International Mother Earth Day, April 22, 2009". Scribd. Iliwekwa mnamo 27 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "In Historic Vote, UN Declares Water a Fundamental Human Right". Democracy Now. Democracy Now. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maude Barlow kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |