Mariano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mariano Díaza(Nyeupe)

Mariano Díaz Mejía (matamshi ya Kihispania: [maɾjano ði.az mexi.a]; anajulikana sana kama Mariano; alizaliwa 1 Agosti 1993]) ni mchezaji wa soka wa Hispania ambaye anachezea katika klabu ya Hispania Real Madrid kama mshambuliaji.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Muda mfupi baada ya kuanza katika klabu ya Badalona mwaka 2011, Mariano alijiunga na Real Madrid, ambako alicheza katika timu C ambapo alikuwa mchezaji bora katika daraja hilo msimu wa 2015-16.

Olympique Lyonnais[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 30 Juni 2017, Mariano alisajiliwa na klabu ya Olympique Lyonnais.Kwa malipo yaliripotiwa kuwa ni milioni 8 .Alicheza kwa mara ya kwanza 5 Agosti katika mechi ya kwanza ya msimu wa 2017-18 Ligue 1 dhidi ya klabu ya Strasbourg, akifunga magoli mawili katika ushindi wa nyumbani kwa magoli 4-0.

Alifikisha magoli 18 kwa msimu wa ligi, na kutengeneza nafasi kubwa ya kuwa mshambuliaji bora pamoja na Memphis Depay na Nabil Fekir.

Rudi Real Madrid[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 29 Agosti 2018, Real Madrid ilitangaza kwamba walikuwa wameshamsaini Mariano kwa mkataba wa miaka mitano (5) kwa ada isiyopungua € 23,000,000.] Alipewa jezi nambari 7 iliyokuwa imevaliwa na Cristiano Ronaldo.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mariano kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.