Maria Eugenia Casar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

María Eugenia (Gina) Casar ni Mmeksiko mtumishi wa serikali ambaye anafanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kitaifa (AMEXCID).[1]

Katika mwaka wa 2020, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, Mpango wa Chakula Ulimwenguni (WFP) Mkurugenzi Mtendaji David Beasley na Chakula na Shirika la Kilimo (FAO) Mkurugenzi Mkuu Qu Dongyu walimteua awe Mshauri Mwandamizi wa WFP kama Msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Assistant Secretary-General level.[2]

Masomo[hariri | hariri chanzo]

Casar ana shahada ya kwanza katika Uhisabu wa Umma, na shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara kutoka Instituto Tecnológico Autónomo de México.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Casar alianza kazi yake kama msomi na akaendelea kuwa kiongozi wa Shule ya Uhisabu na Utawala katika Instituto Tecnológico Autónomo de México.

Casar alifanya kazi katika ngazi ya kitaifa kama; Mweka Hazina wa Kitaifa wa Mexico, Afisa wa Fedha Mkuu katika Banco Nacional de Servicio Financieros; kabla kujiunga na Umoja wa Mataifa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Secta ya benki,Ministry of Finance; and Deputy Vice-President, National Banking Commission in Mexico.[3]

Casar alifanya kazi hapo awali kwa Mpango wa Chakula Ulimwenguni katika Roma alikotumikia kama Katibu Mkuu Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usimamizi wa Rasilimali na Uwajibikaji na Afisa Mkuu wa Fedha (2009-2011), na Afisa Mkuu wa Fedha na Mkurugenzi wa Fedha na Bajeti (2004-2006).

Casar aliwahi kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Mipango, Bajeti na Hesabu, Mdhibiti na Mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa uwekezaji wa mali za United Nations Joint Staff Pension Fund.[3]

Kutoka 2014 mpaka 2015, Casar alikuwa Msimamizi Mshirika waMpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP). Katika jukumu hilo, alimrithi Rebeca Grynspan wa Costa Rica. Kama Msimamizi Mshirika wa UNDP, Casar alishikilia kiwango cha Chini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo Vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Umoja wa Mataifa
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria Eugenia Casar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.