Nenda kwa yaliyomo

Katibu Mkuu wa UM

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mtendaji mkuu wa UM na mwenyekiti wa Ofisi Kuu ya UM ambayo ni kati ya vitengo muhimu vya Umoja wa Mataifa.

Uteuzi wa Katibu Mkuu

[hariri | hariri chanzo]

Katibu Mkuu huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM kwa muda wa miaka mitano. Jina linapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu na Baraza la Usalama la UM. Kwa hiyo uteuzi wa Katibu Mkuu uko mkononi mwa Baraza la Usalama na kila taifa mjumbe wa kudumu linaweza kuzuia jina fulani lisipelekwa kwa njia ya Veto yake. Lakini Baraza la Usalama linapaswa kumteua mtu atakayepata kura za kutosha katika Mkutano Mkuu.

Hakuna sheria juu ya muda wa kazi yake lakini hadi sasa hakuna Katibu Mkuu aliyehudumia UM zaidi ya vipindi viwili au miaka 10. Kuna kawaida ya kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inapita kwenye mabara yote ingawa hiyo si sheria.

Mshahara wa Katibu Mkuu ni dolar za Marekani 176,877 kwa mwaka. (2006).

Orodha ya Makatibu Wakuu

[hariri | hariri chanzo]
# Picha Jina
Muda wa ukatibu wake
Taifa lake Mengineyo Viungo
  Gladwyn Jebb 24 Oktoba 1945 –
2 Februari 1946
Uingereza kaimu Katibu Mkuu  
1 Trygve Halvdan Lie 2 Februari 1946 –
10 Novemba 1952
Norwei alijiuzulu Biografia
2 Faili:Dag Hammarskjold.jpg Dag Hammarskjöld 10 Aprili 1953 –
18 Septemba 1961
Uswidi alikufa katika ajali ya ndege yake huko Rhodesia ya Kaskazini (leo Zambia) Biografia
3 Sithu U Thant 3 Novemba 1961 –
31 Desemba 1971
Burma (leo Myanmar) kazi ya tar. 3 Novemba 1961 hadi 30 Novemba 1962 kaimu Katibu Mkuu Biografia
4 Kurt Waldheim 1 Januari 1972 –
31 Desemba 1981
Austria Veto ya China ilizuia kipindi cha tatu Biografia
5 Javier Pérez de Cuéllar 1 Januari 1982 –
31 Desemba 1991
Peru hakugombea mara ya tatu Biografia
6 Boutros Boutros-Ghali 1 Januari 1992 –
31 Desemba 1996
Misri Veto ya Marekani ilizuia kipindi cha pili Biografia
7 Kofi Annan 1 Januari 1997 –
31 Desemba 2006
Ghana hakugombea kipindi cha tatu Biografia
8 Ban Ki-moon Ban Ki-moon 1 Januari 2007 – Korea Kusini Biografia

Makamu wa Katibu Mkuu

[hariri | hariri chanzo]

Mkutano Mkuu uliamua 1997 kuanzisha cheo kipya cha makamu wa Katibu Mkuu.

Tangu 7 Januari 2007 Asha-Rose Migiro kutoka Tanzania amepewa nafasi hii. Alimfuata Mark Malloch Brown.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]