Nenda kwa yaliyomo

Margaret Singana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Margaret Singana (1938 – 22 Aprili, 2000), pia hujulikana kama "Margaret M'cingana", alikuwa mwanamuziki wa nchini Afrika Kusini.[1]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Margaret Nomvula M'cingana alizaliwa Queenstown, Eastern Cape, binti wa Agnes M'cingana. Mnamo miaka ya 1950, alihama kutoka Queenstown hadi Johannesburg ambapo alipata kazi kama mfanyakazi wa ndani. [2]

Kazi ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Akiwa mfanyakazi wa ndani, Margaret Singana aligunduliwa akiimba wakati wa kufanya usafi. [3] Waajiri wake walivutiwa sana na uimbaji wake hivo walirekodi sauti yake na kutuma rekodi hiyo katika kampuni ya kurekodi. Hivo na walimpa sehemu kama mwimbaji wa kwaya mnamo 1964. "Singana" lilikuwa ni badiliko la jina lake la ukoo "M'cingana", lililokusudiwa kuwa rahisi kwa watu weupe kutamka.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Singana aliolewa na mpiga besi wa jazz Mongezi Velelo. [3] Alifariki Aprili 2000, huko Queenstown, baada ya kuugua kwa muda mrefu [4] na umaskini . [5] Mnamo 2005 kazi yake ilikumbukwa kwa tuzo ya South African Music Awards.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.sahistory.org.za/people/margaret-singana
  2. Max Mojapelo, Beyond Memory: Recording the History, Moments, and Memories of South African Music (African Minds 2008): 87–88. ISBN
  3. 3.0 3.1 Peter Makurube, "Lady Africa is Waiting" Mail & Guardian (18 December 1998).
  4. Margaret Singana – South African History Online
  5. Africa: Farewell To A Golden-Voiced Songstress – AllAfrica
  6. Max Mojapelo, Beyond Memory: Recording the History, Moments, and Memories of South African Music (African Minds 2008): 87–88. ISBN
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Margaret Singana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.