Nenda kwa yaliyomo

Mamphela Ramphele

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mamphela Ramphele

Mamphela Aletta Ramphele (alizaliwa 28 Desemba 1947[1]) ni mwanasiasa, mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi, daktari na mfanyabiashara wa Afrika Kusini.

Alikuwa mshirika wa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi Steve Biko, ambaye alizaa naye watoto wawili. Yeye ni makamu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Cape Town na mkurugenzi mkuu wa zamani katika Benki ya Dunia.[2] Ramphele alianzisha chama cha siasa cha Agang cha Afrika Kusini mwezi Februari 2013 lakini alijiondoa kwenye siasa mwezi Julai 2014. Tangu mwaka 2018, amekuwa rais mwenza wa Klabu ya Rome.

  1. "This is not about me" says DA Presidential Candidate Mamphela Ramphele (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2024-07-13
  2. "Mamphela Ramphele", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-05-30, iliwekwa mnamo 2024-07-13
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mamphela Ramphele kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.