Nenda kwa yaliyomo

Makurunge Kiluvya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makurunge ni mojawapo ya vitongoji vya kata ya Kiluvya katika Wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani.

Jina Makurunge linatokana na miti mikubwa aina hiyo iliyokuwa inapatikana katika eneo hilo.

Vivutio[hariri | hariri chanzo]

Kitongoji hicho ni eneo linalokua kwa kasi sana kutokana na idadi ya watu wanaoendelea kuja kufanya makazi kwa kuona fursa zake kwa wawekezaji kufungua biashara mbalimbali hata viwanda pia. Hivyo Makurunge ina mchanganyiko wa watu wa makabila na dini mbalimbali.

Makurunge ina huduma zote muhimu za kijamii kama barabara ya kiwango cha changarawe kutoka Kiluvya Madukani kuelekea Kisarawe, pia barabara ya kutoka Kiluvya Madukani kuelekea Makurunge Secondary. Barabara hiyohiyo inaelekea chuo cha Sisters of Mary hadi relini. Huduma nyingine zilizopo ni pamoja na maji ya DAWASA na umeme wa uhakika.

Kuna maeneo makubwa yanayoweza kujengwa Viwanda, Masoko, n.k. Pia ni fursa kwa wenye vyombo vya usafiri kuanzisha biashara ya daladala.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Kitongoji cha Makurunge kina shule zifuatazo:

  • Kiluvya “A” Primary School
  • Makurunge Secondary School[1]

Afya[hariri | hariri chanzo]

Makurunge ina huduma zifuatazo za afya:

  • Makurunge Dispensary
  • Mwanyika Dispensary

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Makurunge Kiluvya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.