Nenda kwa yaliyomo

Majira ya kupukutika majani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Majira ya kupuputika majani)
Uzuri wa majani kupuputika katika Green Mountain National Forest.

Majira ya kupukutika majani (kwa Kiingereza Fall au Autumn)[1] ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kiasi. Kadiri ya umbali na ikweta, mchana unazidi kuwa mfupi na usiku kuwa mrefu.

Pamoja na hayo, miti mingi, isipokuwa misonobari na misanduku, inaweza ikapotewa na majani yote: ndiyo asili ya jina la majira.

Kwa Kiswahili majira ya namna hiyo pia huitwa masika.

Yanafuata majira ya joto (kwa Kiingereza "Summer") na kutangulia majira ya baridi (kwa Kiingereza "Winter").

Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.

  1. "Oxford Dictionary on the North American usage of Fall". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-30. Iliwekwa mnamo 2015-04-04.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Majira ya kupukutika majani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.