Majadiliano ya kigezo:Mbegu-muziki

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wazo. Nimeona tatizo upande wa kutaja mwanamuziki na muziki. Kigezo hiki kinajumuisha mambo mawili kwa wakati mmoja. Yaani, mwanamuziki, single, bendi, na kadhalika. Sidhani kama ni wazo zuri kiasi fulani - hasa ikiwa tumeamua kutenganisha makala kwa mtililiko wa majina husika na tendo lenyewe. Nilifikiria kufanya hivi: "Makala hii kuhusu muziki/mwanamuziki fulani bado ni mbegu" badala ya hivi: "Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu". Sikuweka haya juu kwa kufuatia jamii inayoingiza mambo yote hayo ni moja: "Mbegu za wanamuziki" ilhali makala zingine si za wanamuziki, bali muziki au albamu ya muziki. Je, hii ni sahihi kuchanganya makala za muziki na wanamuziki? Wenu kijana mtiifu, Muddyb, au--Mwanaharakati (Longa) 07:11, 29 Juni 2009 (UTC)[jibu]

Nimetofautisha vigezo vya mbegu za muziki na vigezo vya mbegu za wanamuziki. Asante kwa shauri zuri! --Baba Tabita (majadiliano) 13:39, 29 Juni 2009 (UTC)[jibu]
Hongera pia kwa mabadiliko na ujenzi wote ulioufanya!--Mwanaharakati (Longa) 05:03, 30 Juni 2009 (UTC)[jibu]