Majadiliano ya Wikipedia:Mwongozo
eti jina liwe "ukufunzi" au heri mwongozo ? --Kipala (majadiliano) 15:55, 1 Desemba 2009 (UTC)
- Nimetafsiri kadiri kamusi ya TUKI inavyosema. Ukiona si sawa, basi endelea!-- MwanaharakatiLonga 17:01, 1 Desemba 2009 (UTC)
- Nisipokosei Kiing. "tutorial" inaweza kuwa na maana kadhaa. Neno la TUKI inamaanisha aina ya semina kwenye chuo kikuu (nisipokosei). Ila tu je itaeleweka nje ya wanafunzi? Wewe unaonaje "Mwongozo" - je haieleweki kirahisi zaidi? Kama la, tuache. Kama ndiyo: Tuhamishe. --Kipala (majadiliano) 10:03, 2 Desemba 2009 (UTC)
(Yafuatayo yamehamishwa kutoka Majadiliano ya mtumiaji:Muddyb Blast Producer
:Pole mzee Kipala. Dhahili kamusi yako labda ya kitambo! Tazama hii:
tutor n 1 (at colleges, etc) mkufunzi. 2 mdarisi, mwalimu binafsi. 3 (GB) mwalimu wa chuo kikuu, mhadhiri. vt 1 fundisha, funda; darisi. 2 jizoeza, dhibiti, chunga. ~ial adj -a ukufunzi. n semina ya ukufunzi.
Basi hapo ndipo nilipoipata! Hata Wikipedia ya Kiingereza inayo kurasa ya mwongozo (guideline) na hii ya "tutorial-ukufunzi". Kama nilivyosema. Ukiona siyo, basi endelea!-- MwanaharakatiLonga 11:16, 2 Desemba 2009 (UTC)
- Kamusi yangu ileile. Hapa naona: ni maana ya pekee (kawaida kabisa kila neno kuwa na maana mbalimbali ukitafsiri). Nashauri hapo acha kamusi kando - je wewe mwenyewe unaonaje? Neno gani linasaidia hasa? (Jaribu kukumbuka ulionaje ulipoanza wikipedia). --Kipala (majadiliano) 12:28, 2 Desemba 2009 (UTC)
- Sawa. Hamisha tu. Lakini usisahau kama kuna "vikurasa" au "subpages" ambazo zinatumia jina la "ukufunzi"! Endelea tu. Pia, wakati nilivyojiunga, kwangu ilikuwa rahisi kwa sababu nilikuwa ninajua kutumia HTML code kiasa - na vilevile nilikuwa nina nia ya kuweza kutumia na kuchangia Wikipedia. Sijui wao. Labda wapo kwa ajili ya Laptop na zawadi nyinginezo (mzaha!) Basi we endelea tu mzee wangu.-- MwanaharakatiLonga 13:06, 2 Desemba 2009 (UTC)
Hongera mzee Kipala, kwa anzisho la "muundo". Nilishaanza kutoa macho baada ya kusoma yale yaliyomo kwenye ukurasa ule - kule kwenye Wikipedia ya Kiingereza! Haya, tuendelee!-- MwanaharakatiLonga 13:33, 2 Desemba 2009 (UTC)
- Sasa naona mambo yashakuwa mazuri. Hongera kwa kazi ya kutengeneza mwongozo huu. Kila la kheri.-- MwanaharakatiLonga 10:16, 8 Desemba 2009 (UTC)
- NAomba jaribiha hasa hii: Wikipedia:Jedwali. Je inaeleweka? Sijasahau kitu? --Kipala (majadiliano) 13:56, 8 Desemba 2009 (UTC)