Majadiliano:Wafiadini wa Uganda
Mandhari
Naona kama makala hii inataka kujadili habari za "Wafiadini wa Uganda" ipanushwe kidogo kulingana na pande zote zilizohusika yaani Wakatoliki na Waanglikana. Sasa inaonekana kama habari ya upande mmoja tu inayotaja upande mwingine kandokando. Sawa nikiongeza? Kipala (majadiliano) 11:06, 13 Juni 2010 (UTC)
- Suala hilo ni la kweli, nami pia nililifikiria kwanza. Ndiyo maana niliongeza dondoo la Paulo VI ambapo katika kutangaza watakatifu wale 22 waliokuwa Wakatoliki alisema wapo wengine wengi waliokuwa Waanglikana. Hatuna shaka kwamba kila anayemfia Yesu ni mtakatifu, hata asipotangazwa na Papa. Shida ni kwamba tukisema "Wafiadini wa Uganda" kwa maana pana, wapo wengine wengi kabla na baada ya wale waliouawa chini ya Mwanga II. Hata Wakatoliki tuna vijana 2 wenye heri waliofia dini Uganda mwanzo wa karne ya 20. Ni vilevile kuhusu nchi nyingine nyingi. Lakini shida ni kwamba kimataifa tumezoea kuwaita Wafiadini hao (wa Namugongo) kwa jila la "wa Uganda" tu. Sasa uamuzi wako. Usiogope, hatuwezi kusikitika mtu akitangaza sifa za waliomfia Yesu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:03, 14 Juni 2010 (UTC)