Majadiliano:Wachagga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nimejaribu kuratibu makala hii. Kuna bado nafasi ya kuiboresha. Niemacha kwa sasa sehemu juu ya safari za Krismasi lakini sioni maana ya kutaja ya kwamba Wachagga wanasafiri majira ile. Karibu watu wote wa Afrika ya Mashariki hupenda kwenda nyumbani wakati wa Krismasi akikaa mbali. Hasa kwa sababu ni likizo ndefu za Krismasi pamoja na mwaka mpya. Kama huna hoja ni Wachagga wanaozidi wengine katika safari za Krismasi tunahitaji takwimu. Sidhani iko. Uhusiano na mambo ya kukumbuka mizimu na tabia za kichagga haueleweki kama sababu ya kweli ni hasa nafasi yenyewe ya kusafiri. Wakikumbuka au wasipokumbuka watasafiri tu. Naiacha kwa muda nisipoona kitu kipya ningeifuta. --Kipala 19:39, 8 Machi 2007 (UTC)

Majina ya Kichagga[hariri chanzo]

Nasikitishwa kwa kutoorodheshwa jila la SHAYO kama moja kati ya majina asilia ya wachagga.Majina haya yapo sana katika maeneo ya Kilema,Rombo,Old moshi na Uru.Hivyo naomba liingizwe katika majina yalioorodheshwa hapo juu. 82.206.143.68 11:49, 25 Julai 2007

Nimeliingiza. Hata wewe ungeweza kufanya hivyo. Yeyote anayegundua makosa au mapengo anaruhusiwa kurekebisha. --Oliver Stegen 12:44, 25 Julai 2007 (UTC)

Mchagga hali muhogo[hariri chanzo]

Nina mashaka juu ya maelezo ya "wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila". Sina swali kuhusu hadithi hii lakini maelezo yake.

Muhogo ni mmea unaojenga sumu ya sianidi (cyanide) ndani yake kila mahali. Kote duniani unapolimwa watu wana mbinu zao za kuondoa sumu hiyo ama kwa kuiacha kwenye maji kwa siku mbili tatu kabla ya kupika au kulowesha unga wake katika maji kuwa uji inayokaa masaa machache kabla ya kupikwa.

Ninaweza kuamini kabisa ya kwamba watu waliopanda muhogo mara ya kwanza baada ya kuiona kwa majirani walikuwa wagonjwa hadi kufa kwa sababu hawakujua siri ya kuondoa sumu. Lakini siwezi kuamini ya kwamba sumu imo katika ardhi ya Kilimanjaro. Naona sehemu hii isahihishwe au maelezo kamili pamoja na dondoo yafuate. --Kipala (majadiliano) 08:51, 5 Aprili 2008 (UTC)

Sijaelewa mihogo ipi isiyoliwa? Ni hii mihogo tunayouziwa Uswahilini kwetu ama namna gani? Basi na sisi wote tunge kufa, maana wengine kila siku tunashushia chai na mihogo, vipi leo hii mihogo iwe na sumu? Au ile mihogo tunayoipata sisi uku Dar iko tofauti na mihogo inayozungimziwa hapa. Naomba nieleweshwe kidogo.--Mwanaharakati (majadiliano) 12:19, 5 Aprili 2008 (UTC)
Muhogo huwa na sumu ya sianidi ndani yake. Kiwango hutegemea na aina yake. Aina kadhaa kiwango ni kidogo mno haina hasara. Aina tofauti zina kiwango kikubwa zaidi inatakiwa kukaa katika maji kwa muda yanayotoa sumu kabla ya upishi. Natumanini ya kwamba ama wanalima aina zenye sumu kidogo tu kwenu au angalau wanajua kuiandaa vema. Kongo na Afrika ya magharibi wanapokula muhogo zaidi matatizo ya kusumisha yanatokea. --Kipala (majadiliano) 16:17, 5 Aprili 2008 (UTC)
Basi mihogo ya uchagani ndiyo inasumu, lakini mihogo ya Uzaramoni haina sumu kwasababu huwa inakuja mikavu, yaani haija menywa ni mibichi kabisa na wala hakuna ulazima wa kuiweka katika maji kwa muda woworte ule. Nashukuru kwa maelezo yako...---Mwanaharakati (majadiliano) 11:23, 8 Aprili 2008 (UTC)

Kuhusu wachagga na muhogo, ni mojawapo ya hadithi za kijadi zinazosimuliwa na wazee wa kichagga. Ukienda Machame ndani kuna wazee hata wakikuona unakula muhugo mbele yao hawatakubali kuonja maana waamini itawaua. Pia ukizingatia mihogo haikuwa zao lao la jadi, inawezekana waliofanya majaribio zamani walipatwa na janga hilo. Kwa kuwa hakukuwa na vitabu enzi hizo, hadithi zilielezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa mdomo. hivyo ndiyo watu waliweza kujua madawa ya kuwatibu (miti-shamba) na mimea yenye sumu. Ukweli ni kwamba mihogo haiui, hata ikiwa na sianidi ikilowekwa sumu hiyo hutoka.