Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Virusi vya kompyuta

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kirusi si "vya" kompyuta maana hakuna "kirusi cha kompyuta" kwa maana hiyo. Iwe "Virusi ya kompyuta" --Kipala (majadiliano) 19:30, 9 Desemba 2009 (UTC)[jibu]

Loo! It's sound bad! Kwanini? Virus kwenye Kiswahili wanatafsiri kama Kirusi kweli!!! Lakini tukifuata vyombo vya habari na Kiswahili cha sasa kinakubali matumizi ya Virus kwa Virusi bila kutazama wingi kama kwa Kiingereza. Hivyo, jina halina ubaya - ila tu makala hayakupangwa vyema! Ninayo makala hii kwenye kompyuta yangu. Nimeindika vyema kabisa - hivyo nitaiweka pindi nikiimalizia! Salaaaaaaaam!!!--MwanaharakatiLonga 07:21, 5 Februari 2010 (UTC)[jibu]
Duh! Nimependa ongezeko la maelezo yako. Tena umeandika hadi historia yake. Hongera, mzee wangu! Wako,--MwanaharakatiLonga 08:26, 20 Aprili 2010 (UTC)[jibu]
Bado sikio halijakubali "virusi za"... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:12, 19 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Kumbe huogopi ukishambuliwa na "kirusi kimoja" ila tu na "virusi vingi"? Unafanyaje kama "kirusi cha kompyuta kimeandikwa" kwa Kirusi (maana Putin ana watu wengi wanaotunga na kumsambaza virusi)? Je Warusi wanasemaje?Kipala (majadiliano) 20:09, 19 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Hata mimi sikio langu linakataa kabisa "virusi za"--Ndesanjo (majadiliano) 05:45, 20 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Si masikio ya kila Mtanzania tu yanakataa, hata kamusi na serikali: VVU imezoeleka sana. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:56, 20 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Uzoefu wa VVU ni tatizo kweli. Ila tu unatofautishaje kati virusi moja na nyingi? Wengine wameshahariri hapa "kirusi" ambayo inachaganya watu tu! Maana virusi kutoka Urusi ni kweli jambo linalojadiliwa sana kwenye habari za Intaneti. Basi naomba sentensi mifano kwa kutofautisha moja na nyingi. (nitakapotembela tena TUKI nitawauliza, ingawa nitawaona kuhusu mambo mengine) Kipala (majadiliano) 10:13, 20 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Ingawa neno "vita" lina asili ya Kibantu (labda kitenzi ku-kita), si ya Kilatini, linatumiwa na wengi (kamusi nyingine inasema hata kita linakubalika) katika wingi tu kwa kuwa mapigano hayo yanafanyika daima kati ya wengi. Hata virusi havitokei kimojakimoja (hata hivyo kamusi nyingine ina kidahizo kirusi kwa maana hiyo). Kwa kutumia "virusi za" tunaonyesha kwamba Wikipedia yetu inategemea wasio wazawa... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:27, 20 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Naomba utaje kamusi unazorejelea. Halafu nimeomba lete mifano ya sentensi. Inaeleweka lugha mara kwa mara haifuati kanuni za sarufi, na inaonekana "virusi" ni mfano wake. Sipingi. Lakini hatuwezi kukana haja ya kutofautisha umoja na uwingi.
Tukijadili kuhusu magonjwa, tofauti ni kubwa kama virusi fulani huingia mwilini kwa nakala moja-moja zu au kwa wingi ("virus load"). Tukijadili virusi za kompyuta, tunajadili zaidi moja-moja kuliko uwingi. Hupatikana moja-moja (kawaida) lakini hujadiliwa pia ki-makundi au kikabila kutokana na njia jinsi zinavyoendelea. Naomba sentensi zako!
Kuhusu "vita" heri tusichanganye maneno (tutafika kwa "video"). Falsafa hii kuhusu "vita daima" haisaidii ukiandika kuhusu vita mbalimbali. Lakini kama umeshatafakari jambo hili: Kati ya vita nyingi za karne ya 20, Vita Kuu ya Kwanza ilikuwa muhimu hasa kwa Afrika ya Mashariki.- Tafadhali sema sentensi hii kwa namna unayopendelea. Kipala (majadiliano) 15:17, 20 Juni 2019 (UTC)[jibu]

Ndugu, natumaini leo umetulia kuliko jana. Ingawa tunajadili neno "vita" hatuko vitani... Kwanza kamusi zinazotumia neno "kirusi" (tofauti na Kirusi) ni kama vile Kamusi Teule ya Kiswahili na Concise English-Swahili Dictionary. Kuhusu "kita" ni Kamusi ya Karne ya 21 na Kamusi Kuu ya Kiswahili. Hii haikunishi kwamba kwa kawaida maneno haya yanatumika katika wingi. Kamusi zinazotoa mfano wa matumizi sahihi kwamba ni "Vita vikuu" au "Vita vya" ni kama vileː Kamusi Kuu ya Kiswahili, Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Kamusi ya Karne ya 21 n.k. Kuhusu sentensi unayodai, fikiria hii ya kutofautishia umoja na wingiː "Kati ya maji za dunia, ile ya Bahari ya Kifo ina chumvi sana". Kila lugha ina utata wake; fikiria "I love you" (wewe au nyinyi). Amani kwakoǃ --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:45, 21 Juni 2019 (UTC)[jibu]

Asante kwa kutaja kamusi unazorejela. Siwezi kuziangalia hadi wiki 1 maana bado niko Nairobi. Nitatafuta ushauri TUKI nitakapowatembelea tena. Najua kwa kawaida watu wengi hutumia vita kama ki-vi-; kihistoria ilikuwa i-zi- lakini tangu karne ilitazamiwa pia kama ki-vi-. Ila tu sijui matini ambako watu wamejadili vita mbalimbali (ukiandika zaidi na kutofautisha /kulinganisha jinsi nilivyopaswa kufanya katika makala zetu, basi unagonga ukuta huu ambako kamusi jinsi ilivyo siku hizi hazitoi msaada). Hapa ilikuwa ombi langu nisaidie sentensi za mfano. Kwa bahati mbaya mfano wako wa maji haunisaidii kitu. Ukiwa na mfano usio kitendawili nitashukuru zaidi! Kipala (majadiliano) 19:03, 21 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Asante kwa jibu zuri. Mimi mwenyewe sidhani nitasema "kita hiki" au "kirusi hiki", lakini utaona mabadiliko mengine mengi ya ngeli. Kwa mfano sasa hivi neno "mamlaka" liko mbioni kuhamia -ya: tunazidi kusikia "mamlaka haya". Bado kidogo tutasikia "mashine haya". Tunaweza kuzuia kidogo, lakini kama alivyowahi kuandika ChriKo kuhusu "vizuri" hatimaye tutashindwa kushindana na mkondo mkubwa mno wa maji. Kuhusu sentensi yangu, ni kweli niliiandika kwa uchokozi. Ile uliyotaka wewe ni hii: "Kati ya vita vyote vya karne ya 20, Vita Vikuu vya Kwanza vilikuwa muhimu hasa kwa Afrika Mashariki". Amani kwako na unisalimie Wakenya, hasa wanaopendelea Kiswahili chetu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:05, 23 Juni 2019 (UTC)[jibu]
Nimefuatilia majadiliano makali (sio kwa ubaya) na yanayojenga. Niko nyuma kidogo kwenye kwenye kanuni za sarufi. Tusubiri basi tusikie TUKI watasema nini.--Ndesanjo (majadiliano) 02:02, 26 Juni 2019 (UTC)[jibu]