Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Utambulisho wa jinsia

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chanzo cha nadharia

[hariri chanzo]

Bila shaka mada ya jinsia, mabadilikoya jinsi n.k. ni mada ambazo ni jambo gebi katika mazingira ya wasemaji wa Kiswahili. Hata hivyo, inafaa kueleza mada hiyo kama zote kwenye wikipedia yaani bila upendeleo. Chanzo cha utafiti huu na hata jina la "Utambulisho wa jinsia" (gender identity) haikutungwa na "watetezi wa ushoga" bali na madaktari wa saikolojia waliotibu watu waliofika kwao kwa sababu walikuwa na wasiwasi au kuchanganyikiwa kuhusu jinsia yao. ona enwiki: "gender identity was coined by psychiatry professor Robert J. Stoller in 1964 and popularized by psychologist John Money." Kwa hiyo ufunguzi wa makala unahitaji masahihisho. Kipala (majadiliano) 06:50, 22 Januari 2023 (UTC)[jibu]

Hao wawili wanatajwa chini. Kuhusu kutofanya upendeleo, mimi naona wanaofanya upendeleo ni wenzetu wa Wikipedia ya Kiingereza ambao wanazuia mchango wowote usioendana na kilicho "politically correct" huko majuu. Nilijaribu mara kadhaa lakini bure. Hawakubali hata tanbihi tofauti na za wanaotetea kile ambacho wao wanaona ni hakika ya sayansi, kumbe wanasayansi wengine wanakipinga. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:55, 22 Januari 2023 (UTC)[jibu]