Majadiliano:Upatanisho wa imani na sayansi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuna mifupa mingapi katika mwili wa binadamu.

Makala ya mashaka[hariri chanzo]

Makala imeandikwa zaidi kama insha, si makala ya kamusi elezo. Umbo haulingani na kawaida yetu. Tena sehemu "Sayansi imechunguza viumbehai waliopo ..." imenakiliwa neno kwa neno kutoka https://napradck.blogspot.com/2017/11/binadamu-or-human.html. Makala haitoshelezi masharti ya kamusi elezo. Isahihishwa haraka au kufutwa. Kipala (majadiliano) 22:52, 5 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala ya kabla ya mchango huu tayari yalikuwa na sehemu hii inayoonekana kuwa ilinakiliwa kutoka tovuti iliyotajwa. Hata hivyo ingekuwa bora kuondoa matini hii kabisa na kufuatiliza maendelezi hayo na mabadiliko ya tarehe 5/Aprili --Shekeinespere (majadiliano) 20:36, 6 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Ninavyokumbuka, maneno yale niliyatunga mwenyewe katika kuboresha makala iliyoanzishwa na mwanafunzi wetu. Inawezekana mwenye blogu ndiye aliyenakili kutoka ukurasa wetu, si kinyume. Pamoja na hayo, wewe Shekeinespere, usijiamini sana katika kufanya mabadiliko ya kimapinduzi katika Wikipedia hii ambapo u mgeni. Hapa hatuna tabia ya kugongana katika uhariri. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:06, 7 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala yasioandikwa kikamusi-elezi[hariri chanzo]

Makala haya yanakwenda kinyume na kanuni-msingi za Kamusi Elezo huru la Wikipedia kwa kuwa:

(1) Yana mitazamo binafsi ya kidini iliyoandikwa kana kwamba ni kweli zilizodhibitishwa kisayansi au kitafiti na kukubalika kwa misingi hiyo kijumla kwa mfano, kifungu kinachoanza "Jambo la msingi kwa imani ni kwamba vyote asili yake ni Mungu tu aliyeviumba kwa hiari yake." kuendelea (2)Yana madai yasiyo na msingi wowote wa kitafiti kuhusu sababu zinazopelekea mitazamo ya kuwa hakuna Mungu katika baadhi ya wanadamu: "Kwa nini baadhi ya wanasayansi hawaamini kuwa Mungu yupo? Hiyo inatokea kwa sababu sayansi ni ndogo sana kuliko Mungu na haiwezi kuchunguza kila kitu na kupata..." (3) Yana madai sasiyo sahihi kuhusu utenda-kazi na mchakato wa kisayansi, mfano: "Zaidi sana haiwezi kusema lolote juu ya Mungu na kazi yake, kwa sababu si wa ulimwengu huu." Tatizo la kimsingi zaidi ni kuwa yanahitaji kuhaririwa kwa namna ya kikamusi-elezi isiyoegemea upande wowote na isiyofanya madai ya msingi wa kidini kana kwamba ni ukweli halisi wa kisayansi au kifalsafa.--Shekeinespere (majadiliano) 10:02, 7 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Ndugu, wewe una itikadi kali bila kujitambua. Wewe ndiwe unayetaka tukubali sayansi inajua yote, wakati wanasayansi wakuu wanakiri ujinga wao, kwamba kwa mfano fizikia yetu inafahamu kidogo sana ulimwengu ulivyo. Ndiyo sababu inasema kuhusu dark matter n.k. Katika kamusi elezo hakuna kinachozuia kueleza kwamba Waislamu wanamuamini Mungu mmoja au kwamba Wakristo wanaamini Yesu ni Mungu. Hiyo ni imani yao na msomaji anaelimishwa kwamba hao wanaamini hivyo. Katika makala hii inaelezwa kwamba sayansi ina mipaka yake. Haiwezi kusema Mungu yupo wala hayupo: ni nje ya fani yake. Imani za dini zinakubali kwamba kuna njia nyingine za kufahamu, mbali ya utafiti na majaribio ya kisayansi. Makala hii inaeleza pia kwamba wanadini wengi hawaoni mgongano kati ya imani yao na sayansi. Na hiyo inaelezwa pia katika makala za lugha nyingine zilizounganishwa nayo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:37, 7 Aprili 2020 (UTC)[jibu]
Ningependa kudumisha mjadala huu katika mipaka ya lengo la kamusi elezi- bila ya kubishania maoni binafsi au kudharauliana au kutukana - ninakuomba udumishe heshima hiyo hiyo katika mazungumzo. Tulenge mjadala na vipengele vyake - sio wachangiaji kama watu binafsi.

Tatizo kubwa na makala haya ni la "point of view", au mtazamo wa uandishi- ambao unavunja kanuni kuu za kamusi-elezi hii nilivyoelezea. Kosa hili linatokea tena katika mchango wa hivi karibuni zaidi hapa kwenye majadiliano. Naam, baadhi ya sehemu ulizogusia na baadhi ya maelezo uliyotoa hapa yana uandishi unaobainisha kati ya kweli zilizodhibitika kitafiti na yale yanayochukuliwa kuwa kweli ki-imani au kidini. Tatizo ni wakati haya makundi mawili ya uandishi yanaaingiliana. Kwa mfano: "Katika makala hii inaelezwa kwamba sayansi ina mipaka yake. Haiwezi kusema Mungu yupo wala hayupo: ni nje ya fani yake." Sibishani na wazo hili, ninainua hoja kuhusu lilivyoandikwa kwa kuwa huu sio ukweli-halisi wa kisayansi au kimantiki, ila ni moja ya maoni au mitazamo mengi ya kifalsafa - na katika kamusi-elezi, ni muhimu yakaripotiwa vile - jinsi tu ulivyofanya tayari katika sehemu fulani fulani za makala haya. Naomba pia utazame mifano haswa niliyotoa hapo awali ya sehemu haswa za makala ninazoonelea kuwa na tatizo hili, asante. --Shekeinespere (majadiliano) 16:13, 7 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Ndugu, sijaona nimekukosea heshima wapi. Ila uamuzi wako wa kuendelea kufuta karibu ukurasa mzima wakati tupo katika majadiliano ya kuuboresha si sawa. Nimekuambia Wikipedia ya Kiswahili haijazoea vita vya uhariri. Usinilazimishe kukuzuia usihariri. Mimi ni mpenzi wa sayansi, na ninakubali mafundisho yake yaliyothibitishwa. Ujue hilo. Lakini siwezi kuishia hapo, katika uyakinifu. Napenda falsafa na hoja zake na napenda zaidi imani inayopokea ufunuo wa Mungu mwenyewe. Siko peke yangu. Wengi tunafurahi kukubali sayansi, falsafa na imani vilevile bila kuzigonganisha. Katika ukurasa huu, sayansi inasema imegundua nini, falsafa inatoa mchango wake na vilevile imani, bila kuchanganya. Ila pointi kubwa ambayo makala hii kama ile ya Kiingereza inataka kueleza ni kwamba wapo watu wa imani ambao hawabishani na sayansi, tofauti na wanavyofanya wengine wa pande zote mbili. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:00, 8 Aprili 2020 (UTC)[jibu]