Majadiliano ya mtumiaji:Shekeinespere

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Pamoja na salamu hii utaona kwamba mchango wako wa kwanza umeonekana kuwa na kasoro nzito. Hasa A) ulinakili sehemu kubwa ya matini kutoka tovuti nyingine; kunakili ni marufuku hapa. B) hujaleta marejeo yoyote jinsi inavyotakiwa C) umbo haulingani na kamusi elezo. Usipoondoa A) na B) kuna uwezekano mkubwa mkala inaweza kufutwa. Usikate tamaa, uboreshe makala. Ukiwa na swali, karibu! Kipala (majadiliano) 22:57, 5 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Asante kwa ushauri. Kwanza, madai katika swala A) ya kuwa mabadiliko haya yalinakiliwa kwingine sio sahihi. Mchango huu ulielekezwa (sio kutafsiriwa moja kwa mooja au kunakiliwa nje ya wikipedia) na makala ya papa hapa kwenye wikipedia ya "Creation–evolution controversy" katika lugha ya kiingereza. Naomba utoe ushahidi wa unakili unaodai ikiwa upo. Kwa sasa nimerejesha mchango wa awali. Kwa swala la marejeo, hili nitaendelea kulitilia kazi, ila juhudi ya kwanza ilikuwa ni kurekebisha udhaifu wa kimsingi zaidi katika uandishi wa awali wa makala haya kama nilivyoleza katika muhtasari wa mabadiliko hayo.--Shekeinespere (majadiliano) 20:29, 6 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Nashukuru kwa mchango. Ukiona mwenyewe makala yako haiko tayari bado, fuata ushauri katika Mwongozo wetu (Wikipedia:Mwongozo_(Anzisha_makala), kifungu C2). Maanake ukipeleka kazi isiyokamilika katika nafasi ya makala, uwezekano wa kufutwa ni mkubwa. Halafu inaonekana kabisa umenakili sehemu ya nakala. Maelezo yapo kwenye majadiliano ya makala. Sehemu ifuatayo katika makala ni sawa neno-kwa neno ya blogu ya mwaka 2017:
"Sayansi imechunguza viumbehai waliopo duniani sasa na mabaki ya wale waliokuwepo zamani. Hasa baada ya kugundua DNA imeweza kuona uhusiano kati ya hao viumbehai mbalimbali. Hivyo imethibitisha kwamba mwili wa binadamu na ule wa sokwe imetokana na kiumbehai wa zamani (miaka milioni 5 au zaidi iliyopita) katika mlolongo wa mageuko ya spishi."
Blogu https://napradck.blogspot.com/2017/11/binadamu-or-human.html iliandika:
"Sayansi imechunguza viumbehai waliopo duniani sasa na mabaki ya wale waliokuwepo zamani. Hasa baada ya kugundua DNA imeweza kuona uhusiano kati ya hao viumbehai mbalimbali. Hivyo imethibitisha kwamba mwili wa binadamu na ule wa sokwe imetokana na kiumbehai wa zamani (miaka milioni 5 au zaidi iliyopita) katika mlolongo wa mageuko ya spishi."
Kama unaweza kuonyesha jinsi gani hii ilitokea bila kunakili - karibu sana. Menginevyo ni jambo ambalo hapa wikipedia ni marufuku. Ninakushauri ama uondoe sehemu hii haraka sana na kukamilisha matini / marejeo, au uihamishe katika nafasi yako ya mtumiaji (user space) na ukamilishe pale. Hata kama inafutwa hapa una nafasi ya kuipeleka upya. Isipokuwa heri kutafuta lemma nzuri zaidi maana isingebaki vile.
Halafu: kama watumiaji wengine wanaendelea kuhariri makala uliyoanzisha - heri ukumbuke si "makala yako". Tuko wikipedia. Hasa kama umeleta makla isiyokamililika. Ushauri mwema ni kuwasiliana moja kwa moja na wengine (ukurasa wa majadiliano) au kueleza kwenye ukurasa wa majadiliano wa makala kwa nini kupendi kukubai nyongeza (kama nyongeza si bure kabisa, hapa tunaweza kufuta pia hivhivi).Kipala (majadiliano) 06:02, 7 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Naam, kweli kabisa, sasa nimeelewa. Mbeleni nilidhani kuwa tatizo la unakili lilitokea na mchango wa hivi karibuni zaidi niliofanya - ndipo nikaomba ufafanuzi. Hata hivyo, nadhani kuwa mchango nilioweka ulitatua ukosefu wa kimsingi zaidi katika makala haya - yaani kuwa yameandikwa kwa namna isiyo ya kikamusi-elezi. Nadhani suluhu ya kudumu ni kutafsiri makala ya "Creation–evolution controversy" yanayotoa mwongozo na marejeo bora zaidi na yaliyo na mtazamo usioegemea imani au upande wowote katika swala hili. --Shekeinespere (majadiliano) 09:29, 7 Aprili 2020 (UTC)[jibu]