Majadiliano:Tanzu za fasihi simulizi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fasihi simulizi ina tanzu kuu nne(4)

  • hadithi
  • semi
  • ushairi
  • sanaa za maigizo\sanaa za maonesho

hadithi[hariri chanzo]

ni tungo za fasihi simulizi ambazo ni fupifupi zitumiazo lugha ya nadharia.

semi[hariri chanzo]

ni fungu za tungo za fasihi simuliziambazo ni fupifupi zenye kutumia picha tamathali na semi ya ishara.

ushairi[hariri chanzo]

ni fungu la fasihi simulizi linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo yenye utaratibu maalumu.

sanaa za maigizo\sanaa za maonesho[hariri chanzo]

Ni sanaa zinazoambatana na utendaji wa vitendo vya wahusika mbele ya hadhira.mfano michezo ya majukwaani.

sifa za tanzu za fasihi simulizi[hariri chanzo]

  • kufa
  • kuzaliwa
  • kukua.

kila tanzu ina vipera vyake

vipera vya hadithi[hariri chanzo]

  • Ngano
  • Vigani
  • Visasili
  • Tarihi
  • Soga

vipera vya semi[hariri chanzo]

  • Methali
  • Vitendawili
  • Nahau
  • Misemo
  • Mafumbo
  • Lakabu
  • Mizungu

vipera vya ushairi[hariri chanzo]

  • Shairi
  • Utenzi
  • Nyimbo
  • Ngonjera
  • Maghani

vipera vya maigizo[hariri chanzo]

  • Majigambo
  • Vichekesho
  • Kuigiza
  • Mivigha\miviga
  • Ngoma