Majadiliano:Taniaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Maelezo ni kweli hivi? Nikiangalia matumizi yake napata picha kwamba katika isimu inatumiwa sawa na "antonomasia", hapa nukuu kutoka Misingi ya hadithi fupi (Dar Es Salaam University Press, 1992, 237 p.):

"Taniaba - Huu ni usemi unaoonyesha kuwa kitu fulani ni badala ya kitu kingine. F.E.M.K. Senkoro anasema kuwa taniaba ni tamathali ambayo jina la mtu binafsi hutumiwa kwa watu wenye tabia, mwenendo na kazi ya mtu anayefanan-ishwa. Halafu anatoa mifano ya tamathali hiyo kuwa ni:

  • a-Yesu: Dhana ya mkombozi (Raisi Nyerere ni Yesu wa Tanzania)
  • b-Voster: Dhana ya ubaguzi (Mavoster ni wengi katika Afrika hii)"

Tazama HAPA

Je, kuna matumizi nje ya isimu? Kipala (majadiliano) 14:07, 6 Septemba 2020 (UTC)

Leo nimemuuliza mwalimu Mengistu bila kumuambia chochote kwanza. Mara moja amesema taniaba ni ukinzani, akatoa mfano huu: "Si mrefu wala si mfupi". --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:36, 7 Septemba 2020 (UTC)
Baada ya mimi kuona katika kamusi neno "Tabaini", Mwalimu mwingine amekamilisha jibu. Naliingiza. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:22, 8 Septemba 2020 (UTC)