Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Tako la bara

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu "tako" na "kitako" — kuna ulazima wa kutofautisha maana. Kitako cha bahari na "vitako vya bahari" — tuondoe neno matako maana yake ni tofauti kabisa. Hili hutumika viumbe hai kama sikosei msikiko wake katika Kiswahili kutaja kwa kitu kama bahari ama bara ni mtihani mzito.--'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 07:09, 30 Januari 2019 (UTC) [jibu]

Muddyb salaam. Usipopenda "tako la bara" unapendekeza istilahi gani? Kirkeby's English-Swahili Dictionary inatoa "mwambao wa bara". ChriKo (majadiliano) 08:32, 2 Februari 2019 (UTC)[jibu]
Asante kwa onyo. Je Kitako cha Bara ni sawa? Sitaki kusibiri hadi hao wanaotunga vitabu vya sekondari kwa Kiswahili wamefika hapa. Nikichungulia sasa (makala nilitunga miaka mingi iliyopita) kuna "" Kuoza kwa kitako cha tunda (BLOSSOM- END ROT ), hivyo hapa kuhusu kitako cha pilipili hoho, kitako cha pasi. Tuhamishe kwenda "Kitako"? Kipala (majadiliano) 11:26, 2 Februari 2019 (UTC)[jibu]
Mimi sipendi kitako cha bara, kwa sababu kiti hiki ni kikubwa! Musipotaka kuchagua mwambao wa bara, tuendelee na tako la bara basi. ChriKo (majadiliano) 18:58, 2 Februari 2019 (UTC)[jibu]
Wazee wangu, Kipala na ChriKo, nashukuru kwa kunivumilia. Siku hizi nimekuwa mtu wa ajabu sana. Nimekuwa na mambo mengi yananizonga. Nahisi ChriKo ametaja jina la kitaalamu zaidi. Japo ametumia ukali katika kuwakilisha. Kipala, naona tufuate umbo la Chriko—ni bora zaidi!--'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 09:45, 5 Februari 2019 (UTC)[jibu]
Mwambao wa bara? Mwambao ni pale ambako maji na nchi vinakutana, nani ataona sehemu iliyo chini ya maji? Tujaribu kumwomba Riccardo, awaulize walimu wake shuleni. Kipala (majadiliano) 07:09, 6 Februari 2019 (UTC)[jibu]
Mimi binafsi sioni shida kusema "tako la bara", labda ingekuwa "matako"! Mbona kuna "tako la bunduki"? Lakini kana Muddyb anaona shida, tukubali kutafuta mbadala. Walimu wetu wa Jiografia na Kiswahili wamejadiliana na kuhusisha wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka jana. Hakuna jina lililozoeleka. Wao wamependekeza "rafu ya bara" (tafsiri ya maneno ya Kiingereza). Si mbaya. Nikifuata Kiitalia nasema "piattaforma continentale", na platform ni kama "ulingo": au siyo? Uamuzi kwenu na amani kati yetu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:31, 7 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Ninakubali ya kwamba "tako la bara" labda si jina bora. Nadhani swali la Muddy kuhusu "tako" limeshajibiwa: kuna tako la bunduki, tako la tunda, tako la ua, nimekuta pia tako la pasi. [CSED: tako 1. buttock, posterior. 2. butt-end of anything such as gun, bowl; the base of anything; TUKI SED: tako nm ma- [li-/ya-] 1 buttock, behind, rump. 2 butt, base (of something); Kamusi Kuu: tako b. sehemu ya chini ya kitu ambayo hutumika kukikalisha kitu hico chini au juu ya uso wa kitu kingine ]

- "Mwambao" sidhani inaweza kufaa, maana inataja sehemu ya nchi inayoonekana kando la maji. "Mwambao wa Afrika ya Mashariki" kamwe ni eneo lililo chini ya maji.

Sasa "rafu". Hmm. Ni tafsiri ya moja kwa moja ya "shelf" ila tu kwa maana gani? Sina uhakika. Nilijifunza neno "rafu" kwa kutaja kitu kama kabati isiyo na milango, kama rafu ya vitabu yenye bao kadhaa (na kamusi zangu zinaeleza vile, kwa kutumia majina kabati, kisanduku, . "Shelf" ilichaguliwa na wanajiografia kwa maana ya "en:cornice" yaani sehemu ya jengo linaloenea nje ya ukuta. Je rafu inaeleweka vile? Kipala (majadiliano) 07:37, 12 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Shelf maana yake ya kwanza ni kitu tambarare, ndiyo sababu kinatumika kwa ajili ya kutunzia vitabu n.k. Kwa msingi huo neno lilitumika kuhusu bara, ni kama linakalia rafu. Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:10, 12 Februari 2019 (UTC)[jibu]