Majadiliano:Sentensi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Chanzo ?[hariri chanzo]

Nimeona chanzo cha makala ni kizito kidogo. Vipi kuanza makala hivyo? Sentensi ni idadi ya maneno yaliyopangwa pamoja kufuatana na kanuni za sarufi kwa kusudi la kuwasilisha habari fulani.

Kwa lugha nyingine ni kipashio kikubwa cha kimuundo ambacho kimeundwa na kirai nomino(KN) na kirai kitenzi(KT) ambacho hutoa taarifa fulani. Kimsingi kirai nomino kina miundo mbalimbali katika lugha ya Kiswahili. Kipala (majadiliano) 18:57, 7 Julai 2014 (UTC)

Salaam. Makala nimeikuta. Nimeongeza yangu. Ila hata mie sijapendezewa na muundo wa mwandishi wa awali. Hivyo nilikuwa natafuta njia mbadala ya kuboresha mwanzo wa makala. Nilitegemea kufanya hivyo nikiwa ofsini - jana nilikuwa nyumbani na intaneti ilinisumbua sana. Si vibaya ukisawazisha mzee wangu. Ukiangalia historia utaona kama si mimi niliyeandika hayo! Wako,--MwanaharakatiLonga 05:42, 8 Julai 2014 (UTC)