Majadiliano:Ring'wani

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mtumiaji mwenye anwani ya IP namba 196.45.158.87 ameongeza maelezo kuhusiana na kata ya kijiji hiki. Hili pia lilikuwa tumaini la mzee Kipala, kwamba ipo siku mmoja kati walioishi kwenye vijiji hivyo - wataongeza masuala fulani. Amechangia vizuri, lakini hakupangilia vyema kama jinsi inavyotakiwa, nami bila hiyana nikasawazisha kama inavyopaswa! Basi hongera kwa mzee Kipala aliotoa wazo la kuanzisha makala hizi za kata za Tanzania!!--Muddyb MwanaharakatiLonga 10:13, 21 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

MAKANUSHO JUU YA UONGO ULIOWEKWA NA MWANDISHI KUHUSU RING'WANI[hariri chanzo]

Ndugu wasomaji kuna mwandishi hapo juu kajaribu kuihadaa jamii na wadau wote wa mtandao kuhusu Ring'wani na hata kufika mahala akaanza kuzisifa familia za Ruge kuwa ndio Ring'wani na kushindwa kabisa kuweka taarifa sahih kuhusu kijiji hiki, hivyo basi namtaka aibadilishe taarifa yake,,,

Ndugu, asante kwa mchango wako lakini hueleweki. Kwanza unammaanisha "mwandishi hapo juu" gani? Ana jina je? Au unamlenga mhariri asiyejiandikisha? Halafu unadai kuna uwongo basi naomba utupe maelezo 1) habari gani si sahihi ?? na 2) habari gani unaona ni sahihi? Kipala (majadiliano) 20:02, 1 Aprili 2015 (UTC)[jibu]