Majadiliano:Orodha ya shule nchini Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Orodha hii ni ya lini? Kwa mfano, usajiri Alfagems Secondary School ni wa mwaka 2008, lakini haimo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 04:11, 26 Februari 2017 (UTC)

Uzuri wa Wikipedia, unachokiona hakipo, unaongezea! Hata shule ya msingi Kiwalani haijakuwepo - mahali ambapo mimi nimesoma. Shule ya Yombo na Kiwalani ni shule ambazo zipo tangu sabiini mwanzoni... Nimeongeza kwenye orodha. Hata wewe unaweza mkuu...Ndiyo dhumuni hasa--MwanaharakatiLonga 11:15, 26 Februari 2017 (UTC)
Si vibaya kuorodhesha shule - ingawa kama unataka pia shule za msingi unapaswa kuunda orodha za wilaya au tarafa! Hata hivyo naomba tusiendelee kuunda makala kuhusu kila shule maana hapa tunapata tatizo la Wikipedia:Umaarufu, ambayo haipatikani kwa shule nyingi.
Tufuate mashariti ya kimsingi ya umaarufu, kama vile Wikipedia:Umaarufu#Kanuni_ya_kimsingi_kuhusu_umaarufu_kwenye_Wikipedia:
  • Mada (au mtu) inastahili makala kama masharti matatu yanatimizwa:
    • imeshajadiliwa katika jamii kwa kiwango fulani (si mara ya kwanza hapa wikipedia!)
    • katika vyanzo vinavyoweza kutegemewa (si facebook, twita, tovuti ya binafsi tu)
    • tena vyanzo visivyotungwa na wenyewe (si tovuti ya wenyewe, matangazo yao).
Maana kama hatuna ushuhuda nje ya facebook au tovuti ya wenyewe au kutajwa kwa jina tu katika orodha fulani - hatuna umaarufu wa kutosha. Nashauri tusiendelee kuunda makala hizi pasipo na ushuhuda imara zaidi. Kipala (majadiliano) 19:07, 21 Agosti 2019 (UTC)