Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Mtindo wa Kiroma

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wazo: kwanini makala isiwe na jina la "Ujenzi wa Kiroma" badala ya "Mtindo wa Kiroma"? Sipati maana ya kina pindi nitazamapo picha zilizopo ikiwa ni pamoja na maelezo yake. Tafakari!--MwanaharakatiLonga 05:10, 8 Agosti 2011 (UTC) [jibu]

Tunatafuta pamoja misamiati ya kufaa. Uliopendekeza unawezekana. Mbadala wake ni "Usanifu majengo wa Kiroma". Lakini wengine wanaweza kupenda mingine tena. Karibuni! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:00, 8 Agosti 2011 (UTC)[jibu]
Ah, Riccardo! Huoni kama unaweka sentensi ndefu sana kwa kunadika "Usanifu majengo wa Kiroma"? Ujenzi wa Kiroma ni fupi na inataja maana zote. Unaonaje?--MwanaharakatiLonga 10:20, 8 Agosti 2011 (UTC)[jibu]
Tutafakari tena. "Mtindo wa Kiroma" si vibaya sana, maana ile "romanesque" inataja hasa majengo lakini pia kipindi cha sanaa (uchoraji) nisipokosei. "Ujenzi wa Kiroma" au "usanifu majengo wa Kiroma" kwangu pana mno; ningetegemea zaidi kusoma juu ya usanifu wa Waroma wa Kale au usanifu jinsi ulivyo kawaida Roma mjini. Lakini hapa ni mtindo wa ujenzi uliotumia sehemu za usanifu wa Waroma wa Kale; jina hili lilitungwa karne nyingi baadaye na wataalamu wa karne ya 19. Yaani haikuwa ya Waroma wenyewe lakini mtindo ulitumia sehemu za usanifu w Waroma wa kale... Kipala (majadiliano) 21:38, 8 Agosti 2011 (UTC)[jibu]