Majadiliano:Mkono

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ah, sijaona tatizo bado. Naona lugha imekaa vyema kabisa. Labda twende mahali pengine?--MwanaharakatiLonga 09:31, 11 Aprili 2011 (UTC)

Kusita kwangu ni namna ya kutaja mkono kwa maana ya "hand" - hii kwa lugha za Ulaya ni sehemu kuanzia kiwiko pamoja na vidole. Nimeweka hapa "kiganja" lakini nikichungulia kiganja labda ni uwazi wa ndani tu, bila vidole na bila kumaanisha sehemu ya nyuma yake. Ungesemaje kile ambacho kwa Kiingereza ni: "In the accident he lost the right hand and the left arm?" Halafu maskini jirani "lost the left foot and the right leg"? Inawezekana kusema: kiganja cha kulia kilikatwa kwa upanga kikaanguka chini? (kama ni "hand" - sawa; kama ni "palm" pekee - haiwezekani.) Kipala (majadiliano) 18:47, 11 Aprili 2011 (UTC)
Kipala, hapa unatumia kiwiko kwa kusema "wrist", lakini kwenye mchoro maana ya kiwiko ni "elbow". Maana gani ni sahihi? KAST inasema ni "wrist". ChriKo (majadiliano) 16:37, 27 Februari 2021 (UTC)
Hapo nisingeenda tena na KAST ambayo ni ya 1995. Natumia sasa (sikuwa nayo 2011) KKS (nikiangalia pia Kamusi Kuu) ha hii inasema "Kiwiko /kiwiko/ nm (vi-) [ki-/vi-] kiungo kinachounganisha kiganja na sehemu ya juu ya mkono, agh. panapovaliwa saa;kivil". Kwa hiyo naona hata "kiwiko" kimepata jibu.
Pamoja na hayo naona ni Kiswahili kibaya chini, ni moja ya makala zilizotungwa kwa kutumia google translate.Kipala (majadiliano) 17:08, 27 Februari 2021 (UTC)
Kwa hivyo hakuna neno moja kutaja "wrist"? Lazima tutumie kifundo cha mkono? ChriKo (majadiliano) 19:02, 27 Februari 2021 (UTC)