Majadiliano:Marambo

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Picha hainonyeshi mahali pa Tanzania bali ya Malawi / Nyasaland. Maelezo ya picha kwenye commons ni kosa. "in the Marambo" inaonyesha si kijiji kimoja lakini ni eneo. Linganisha Politics and Christianity in Malawi, 1875-1940, by John McCracken, uk. 165, anaposema "the Marambo (the Luangwa valley)". Pia andishi "Livingstonia" linadokeza ni picha kutoka wamisionari wa Kiskoti wa kituo cha Livingstonia kilichopo Malawi, na hao Waskoti wa Free Church Mission hawakuingia katika Tanzania mwaka 1910 maana hii ilikuwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza.

Nashindwa kusahihisha commons kutoka mahali nilipo kwa sababu hapa wanazuia commons naweza kuingia kwa proxy tu lakini proxy inazuiliwa kusahihisha kwenye wikipedia. Naomba yeyote asahihishe huko. Kipala (majadiliano) 20:08, 25 Novemba 2015 (UTC)[jibu]