Majadiliano:Krismasi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nime soma makala ya kuhusu krimasi kwa kweli tusifundishe watu kwa yesu alizaliwa tal 25 mwezi wa 12 isyo kweli hivi tuna weza kujiuliza kuwa kwa nini watu hupenda kusema uongo wakati biblia imekataza? jambo hili linapaswa tujiilize sana. ukweli kwamba yesu hakuzaliwa siku hiyo na hata hajawahi kuwambia watu washelehekee siku hiyo wala wazazi wake wakati waka hai huja ona kama walikuwa wakishelehekea sikukuu hiyo pia hata mitume hawakuwahi kufanya hivyo sasa je hii siyo ibada ya kujitungia kama tuna tunga ibada zetu tutakwenda motoni.'mimi ni mwalimu philipo sachi E-mail sachiphilipo@yahoo.com

Bwana Sachi naomba kwanza ujiandikishe katika wikipedia fungua akaunti; pili si busara kubandika email yako hapa; tatu naomba soma makala halafu andika baadaye kama bado una neno. Ninavyosoma mimi makala inasema waziwazi "Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa." - Imani yako juu ya kwenda motoni au wapi haituhusi hapa wikipedia maana hapa tunakusanya elimu yaani habari zinazoweza kuthebitsishwa hivyo unakuta hapa habari juu ya imani (lakini si mahubiri ya imani) na habari za kihistoria zilizothebitishwa au habari zinazojadiliwa na wataalamu bila mapatano juu ya yale yaliyotokea tukijaribu kuonyesha pande muhimu ya mjadala huo wa kitaalamu. Wasalaam Kipala (majadiliano) 15:15, 15 Desemba 2010 (UTC)[jibu]

Nimeondoa sehemu ya "Krismasi katika maisha ya watu" maana ilikuwa zaidi kama mahubiri si maelezo ya kamusi elezo. Kipala (majadiliano) 10:33, 23 Desemba 2012 (UTC)[jibu]

Sol Invictus[hariri chanzo]

Naona sehemu hii iandikwe tofauti; nikiona majadiliano ya wanahistoria, hakuna uhakika kama kweli kulikuwa na sikukuu muhimu ya Sol Invictus. Pia ushuhuda wa imani katika tarehe 25 Disemba unapatikana tangu mwaka 200 hivi kutokana na maandiko ya Hippoliti. Ona

Kwangu hakuna shida. Ukiwa na hakika, badilisha tu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:24, 24 Desemba 2022 (UTC)[jibu]