Majadiliano:Kong'oli
Mandhari
Maneno yasiyokuwa na maana maalumu. --Mwanaharakati 14:49, 25 Oktoba 2007 (UTC)
- Naelewa makala yasema kwamba kuna watu wanaotumia neno hili badala ya "kubofya" - sivyo? Kama ni kweli - basi. Sioni ulazima wa kuwa na makala hii lakini tuko wachache vile sipendi kumkatisha mtu tamaa akiandika makala ninayoona mimi haina maana sana. Makala labda ina faida ndogo lakina haina hasara kwa hiyo ibaki.
- Nikitazama makala zetu nina hofu kuhusu makala zetu zinazohusu dini kwa sababu hapa tumepata wahubiri wa kikristo pia wa kislamu wanaoeleza habari zao za kidhehebu kama ukweli halisi. Yaani sina neno na mhubiri maadamu nahubiri mimi mwenyewe nikiwa Mkristo lakini katika kamusi elezo hatuhitaji mahubiri ila maelezo yanayoeleweka na kulingana na utaalamu kwa kueleza pande mbalimbali. Kwa hiyo nikikusanya pumzi yangu kabla sijanirusha katika uwanja huo sina hamu kuvutana kuhusu makala kama kong'oli. Lakini wewe ni huru kuisahihisha unavyoona. Labda kuingiza category:lugha ya compyuta ?? --Kipala 15:40, 25 Oktoba 2007 (UTC)
- Leo hii, nime-google "kong'oli tovuti" (ilitokea mara 4,600) kulingana na "bofya tovuti" (ilitokea mara 33,500). Ninavyoona, maneno yote mawili humaanisha tendo moja. Kwa vyovyote tungehitaji marejeo au viungo vya nje kwa ajili ya kuthibitisha maelezo humo, sivyo? Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 13:39, 19 Oktoba 2009 (UTC)
- Poleni. Sidhani kama maneno haya yanapatikana kwa "marejeo." Hayo, ni maneno ya msimu tu na msimu wake ukipita basi. Hakuna tena haja ya kutumika. Sioni sababu ya makala hii kuwepo. Sijui wenzangu.-- MwanaharakatiLonga 16:26, 19 Oktoba 2009 (UTC)