Kong'oli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kong'oli ni neno litumikalo katika mtandao. Linatumika kuashiria kitendo cha kufungua tovuti tofauti kwa kubonyeza puku ya tarakishi. Watu wengi zaidi hutumia neno la kubofya kwa tendo hilohilo. Kwa upande mwingine neno la kong'oli si rasmi sana.

Historia ya Kongo'li[hariri | hariri chanzo]

Mara ya kwanza, neno la kong'oli lilitokea katika kipindi cha televisheni kilichokuwa kinaitwa "RADI" kilchokuwa na wasanii wa Kaole Sanaa Group. Katika moja kati ya maigizo yao kulikuwa na mwigizaji mmoja aitwaye Jackson Makweta maarufu kama "Bambo". Huyu bwana ndiye aliyekuwa anasema "Kong'oli" akimaanisha "kupiga". huyu bwana bambo alikua akiigiza lafudhi ya kiswahili iliyoathirika na lugha za watu wa kusini hasa songea, mfano, kabila la wanyasa, wangoni, wamatengo hata na wapogoro wa kusini mwa morogoro, wao wanakawaida ya kutamka kwa kubadlisha silabi ya mwisho ya neno lolote kuwa "li". hivyo basi neno kong'oli lina asili ya neno "kong'ota", (kt [ele] 1 tap lightly, beat lightly. 2 punish (by beating);)hivyo bwana bambo yeye alikua akitamka hivyo lakini akimaanisha kong'ota. Akiwa anataka kusema "nitakupiga" yeye husema "Nitakukong'oli", k.m. na rungu au chupa. Mara nyingi akisema hivyo huwa anatumia silaha. Mazoea yaliendelea hadi ikawa ni kawaida kwa wananchi kusema "nitakukong'oli" mara tu wanafanyapo utani. Baadaye watu wa mtandao wakaanza kutumia maneno haya kwa ajili ya maana maalumu ilivyoelezwa hapo juu, hasa watu wa mtandao wa "Darhotwire", mtandao wenye kuzungumzia maisha ya vijana wa Tanzania hasa katika nyanja za sanaa n.k.

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kong'oli kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.