Majadiliano:Kenneth John George
Mandhari
Nashauri kuangalia makala hiyo upya. Kitaaluma na kikazi mhusika ni mtaalamu wa bahari, somo lake ni elimu ya bahari. Makala ya Kiingereza haionyeshi kama aliwahi kusoma habari za lugha au isimu; kwa hiyo inafaa kutaja kwanza elimu yake ya bahari, na mafanikio yake katika ushairi na isimu kwenye nafasi ya pili.
Halafu makala ya enwiki haitaji kwamba alitoa vitabu 8 kwa lugha za Kikelti, inataja tu idadi ya michango aliyotoa kuhusu lugha hizo, pamoja na idadi ya ushairi kwa lugha ya Kicornwall.
Hakuna dalili kwamba alitengenezwa sanamu yoyote jinsi makala inavyodai. Sehemu inayotaja kazi yake ya elimu ya bahari imebaki na istilahi za kiingereza zisizotafsiriwa; numerical modeling si "ufundi". Kipala (majadiliano) 07:31, 31 Mei 2023 (UTC)
- sawa nilifanya utafiti wangu mwenyew na kusoma baathi ya marejeo mbalimbali na nikaandika naona kwenye kingereza ni tofauti basi nitarekebisha kufuata lugha ya kingereza Hussein m mmbaga (majadiliano) 07:51, 31 Mei 2023 (UTC)