Kenneth John George

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kenneth John George

Kenneth John George ni mtaalamu wa bahari, mshairi kutoka nchini Uingereza anaishi Cornwall na anazungumza lugha ya Breton, Kiingereza na Kifaransa. George amechapisha zaidi ya vitu nane vinavyohusiana na lugha ya Kiselti ikiwa ni pamoja na kamusi za lugha ya kiselti. George alikuwa mwalimu wa elimu ya bahari katika Chuo Kikuu cha Plymouth.

Kenneth ana machapisho zaidi ya hamsini kuhusu elimu ya bahari ikiwa ni pamoja na kitabu cha mafunzo kuhusu maji kujaa na kupwa baharini ambacho kimeuza nakala zaidi ya 1000. George ni mjumbe wa kamati ya wawakilishi wa shirika la Kesva na Taves Kernewek (Bodi ya Lugha ya Cornish) ambalo linaendeleza lugha ya Cornish. George alistaafu mwaka 2006 na kuanza kujifunza lugha ya Kijapani.[1][2][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Dr. Ken J. George - research sea shelf oceanography plymouth. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-02-10. Iliwekwa mnamo 2023-05-31.
  2. Bywnans Ke Published. Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-07-04. Iliwekwa mnamo 2023-05-31.
  3. Who We Are.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kenneth John George kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.