Majadiliano:Jahazi Modern Taarab

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nimerejesha ongezeko la nyimbo za Jahazi kwasababu pale sio mahala pake. Kwa kawaida viungo vya nje kwa nyimbo huwekwa katika makala ya nyimbo. Kwa mfano, lile ongezeko lilitakiwa liwepo katika makala ya "Two in One" Single na sio makala ya Jahazi. Sijui ni kwanini huwa hivyo, lakini ndiyo ninavyoona kwa wenzetu! Aisijisikie vibaya kwa hilo na kama akiweza, basi aanzishe ukurasa wa nyimbo ya Two in One. Hapo ndipo ataweza kuandika yote kuhusu Jahazi na Youtube. Ikionekana nimekosea, basi irejeshwe!!!--Mwanaharakati (majadiliano) 07:29, 13 Septemba 2008 (UTC)[jibu]

Samahani Muddy lakini isingekuwa vema kuacha viungo vya nyimbo kwenye ukurasa wa bendi? Yaani watu wakitaka kusikia bendi moja kwa moja waende wapi? Sijui kama tutapata makala hizi zote kuhusu kila wimbo ; hata kama inaandikwa basi tutaona kiungo hiki mara mbiloi. Lakini kwa jumla naona ingeboresha makala ya bendi tukiwa na mifano michache ya uimbaji pia. Tazama makala yako juu ya Frédéric Chopin uliona vema kuweka viungo kwa mifano ya muziki yake na mimi niliipenda. --Kipala (majadiliano) 10:11, 13 Septemba 2008 (UTC)[jibu]
Ni sawa kabisa unavyosema. Lakini mara sehemu za viungo vya ndani huwa haiwekewei viungo vya nje. Hata mimi najua kama hawa Jahazi wanabaadhi ya video zao katika Youtube, lakini sikuchukua hatua kwa kuwa naamini kuwa kutaja nyimbo za mwanamuziki katika sehemu ya internal link haileti maana. Labda katika viungo vya nje. Pia nilishapanga kuwa nitatumia viungo vile pindi nitakapoumba makala ya albamu ya "Two in One (albamu)", huko ningeweka viungo vya Youtube na sio katika makala kuu ya Jahazi! Sijui nimeeleweka hapo?--Mwanaharakati (majadiliano) 05:07, 15 Septemba 2008 (UTC)[jibu]
Nakubali kuhusu viungo vya ndani na nje. Ni vema kuweka mifano ya uimbaji kwenye viungo vya Nje. --Kipala (majadiliano) 07:47, 16 Septemba 2008 (UTC)[jibu]