Majadiliano:Benedikto Mwafrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

=Mwafrika wa kwanza??[hariri chanzo]

Nina wasiwasi juu ya sentensi ya kwanza katika makala. Inasema Benedikto alikuwa mwafrika mweusi wa kwanza aliyetangzwa mtakatifu katika kanisa katoliki.

Sasa Wajerumani na Waswisi wanajua watakatifu mbalimbali waliokuwa Waafrika. Anayejulikana hasa ni Mt. Morisi anayesemekana alikuwa mwafrika mweusi kutoka Nubia (kusini ya Misri na kaskazini ya Sudan) aliyekuwa afisa wa kikosi cha wanajeshi Waroma kilichoitwa "kikosi cha Thibai" kufuatana na mji wa Misri kusini. Kati ya askari wa kikosi chake walikuwa Wakristo wengi waliouawa mnamo mwaka 300 baada ya kukataa sadaka mbele ya miungi wa Kiroma kwa sababu ya imani yao ya kikristo. Morisi mwenyewe pamoja na wengi katiy a wenzake wanaaminiwa kuwa Waafrika wesui jinsi walivyo watu wa Nubia. Wanakumbukwa hasa kama watakatifu katika maeneo ya Uswisi na Ujerumani walipouawa.

Pia nina wasiwasi juu ya matumizi ya neno "mnegro". Sidhani ya kwamba inaeleweka pia sidhani ya kwamba inasaidia maelewano. --Kipala (majadiliano) 17:50, 27 Aprili 2009 (UTC)