Maiduguri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mahali pa Maiduguri katika Nigeria

Maiduguri ni mji mkuu wa jimbo la Borno nchini Nigeria. Mji ulianzishwa mwaka 1907 na Waingereza kama kituo cha kijeshi.

Leo hii kuna wakazi 2,000,000. Kuna Chuo Kikuu, mahospitali, masoko, uwanja wa kimataifa wa ndege. Tangu 1974 reli ya Nigeria imefika mjini.

Miaka ya nyuma palikuwa na fitina kati ya Wakristo na Waislamu mjini. Waislamu ni wengi mjini penyewe na upande wa kaskazini ya Bornu; Wakristo huwa wengi upande wa kusini. Hasa baada ya habari za machoro ya Mtume Muhamad huko Denmark kufika Borno yalitokea mashambulio ya vijana Waislamu dhidi ya Wakristo